SH BILIONI 1.8 KUKOPESHA WAJASIRIAMALI WANAWAKE,VIJANA,WALEMAVU ZANZIBAR

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kupitia Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) imetenga Sh Bilioni 1.8 kwa ajili ya kutoa mikopo kwenye  vikundi vya wajasiriamali wanawake,vijana na walemavu ili kuweza kuwainua kiuchumi kwakuboresha biashara.

Mikopo hiyo itakayotoka kwa njia ya vikundi vya watu wasiopungua kumi itatolewa  na ZEEA kwakushirikiana  Benki ya Biashara Tanzania (TCB)  ambapo awamu ya kwanza itawafaidisha wajasiriamali  750 waliopo kwenye vikundi 75.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Agosti 2, 2024  wakati wakusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya TCB na ZEEA, Mkurugenzi Mkuu wa ZEEA Juma Burhan Mohamed amesema lengo la mikopo hiyo ambayo  ni asilimia kumi ya mapato ya halmashauri zilizopo visiwani humo ni kupunguza tatizo la ajira kwakuwa kupitia fedha hizo watu watajiajiri na kujipatia kipato.

“Utaratibu wa fedha hizi tutakuwa tunaziweka kadri tutakavyokuwa tunazipata kutoka katika vyanzo vyetu,awamu hii ya kwanza tumetenga Sh  Bilioni 1.8 kila baada ya miezi mitatu tutakuwa ,utaratibu uliopo kila kikundi kitapata mikopo kuanzia Sh Milioni moja mpaka Sh Milioni 30,miikopo hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira,mikopo hii haina riba”amesema Mohamed.

Amesema ZEEA pamoja na TCB wamejipanga kutoa mikopo hiuo na kuweka utaratibu mzuri wakimifumo ambayo inasomeka pamoja na kanzi data itakayokuwa inatoa taarifa kwa    wananchi kuhusu mikopo yao.

 Amesema mikopo itaanza kutolewa mapema wiki ijayo na kwamba mpaka sasa ZEEA imeshawasilisha vikundi 34 vya awali katika benki ya TCB kwa ajili yakuanza mchakato wa utoaji wa fedha hizo.

Awali Mkurugenzi Mkuu TCB Adam Mihayo amesema utoaji sahihi wa mkataba huo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinsuzi (SMZ) Dk.Hussein  Mwinyi  ambapo aliitaka TCB kuwa kichocheo na kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya Zanzibar.

“Baada ya maagizo hayo tukaweka mkakati wa miaka mitano ambapo katika mpango mkakati wa miaka mitano tukasema tutachochea uchumi wa Zanzibar,leo kupitia makubaliano na kutokana mtandao wetu mpana wa matawi Unguja na Pemba tutaenda kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na wenye ulemevu,”amesema Mihayo.

Amesema katika utoaji wa mkopo hiyoasilimia 40 ya fedha zilizotengwa zitaenda kwa wanawake,asilimia 40 vijana huku asilimia 20 iliyobaki itapelekwa kwa walemavu.

“Mikopo hii riba yake itakuwa sifuri tumepanga tutoe kwa vikundi 75 kila kikundi kitakuwa na watu kumi sawa na watu 750 tutaenda kupanua wigo wakuondoa tatizo la ajira tutumia teknolojia ,tunaamini tutaweza kupeleka huduma kwa haraka kwa makundi yote,”amesema Mihayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *