taifatz

AWESO ATOA UHAKIKA WA HUDUMA DAR NA PWANI

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha inafanya maboresho kwenye mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu hususani pampu za kusukuma maji ili kuwezesha huduma ya maji iweze kupatikana kwa ufasaha na kwa wananchi wote. Mhe. Waziri ametoa maagizo…

Read More

Maandalizi muongozo mpya wa elimu yapamba moto

*Shule 96 za sekondari zasajiliwa kutoa mafunzo ya amali Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema hakuna mwanafunzi atakayeshindwa kujiunga na sekondari kwa sababu ya ufinyu wa miundombinu ifikapo mwaka 2028 kwakuwa imeshafanya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa mikondo miwili ambao watamalizia elimu ya msingi mwaka 2027. Wanafunzi hao ambao ni…

Read More

MAONESHO YA UTALII YA ITB-UJERUMANI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi zawadi  Rais ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Utalii Duniani (World Travel and Tourism Council-WTTC) Julia Simpson mara baada ya kikao cha kujadili namna ya kushirikiana kutangaza utalii, kilichofanyika katika banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Utalii  ya ITB jijini Berlin, Ujerumani leo…

Read More

ACT Wazalendo walia ukatili kwa mtoto wa kike

Chama cha ACT Wazalendo kimetoa wito kwa Serikali na vyombo vyake vya dola kupunguza muda wa uendeshaji wa kesi za ukatili dhidi ya watoto na wanawake. Chama hicho kimependekeza muda wa uendeshwaji wa mashauri hayo usizidi miezi miwili hadi kumalizika kwake ili haki ionekane kutendeka. Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 11, 2023 jijini Dar es…

Read More

Dk Biteko ashiriki Rombo Marathon, apongeza ubunifu wake

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo ameshiriki mashindano ya Rombo Marathon yaliyohusisha mbio za Kilometa tano, kumi na 21 na kupongeza waandaaji kwa ubunifu wao uliopelekea marathon hiyo kuendelea kuimarika kila mwaka ambapo licha ya kulenga katika kuimarisha afya kwa washiriki, imejikita katika kuchangia uboreshaji wa huduma mbalimbali za…

Read More

Kiongozi wa upinzani aliyechomwa kisu shingoni Korea Kusini ahamishwa hospitali

KIONGOZI wa chama cha upinzani cha Democratic Party cha Korea Kusini, Lee Jae-myung amewahishwa hospitali mjini Seoul baada ya kuchomwa kisu shingoni na mtu asiyejulikana. Shambulio lilitokea wakati Lee alikuwa akikagua eneo lililopendekezwa kufanyika ujenzi wa uwanja wa ndege mpya huko Busan. Mshambuliaji aliyevalia taji la karatasi lenye maandishi “Mimi ni Lee Jae-myung,” kwanza alikaribia…

Read More

Mchinjita autaka umakamu mwenyekiti ACT- Wazalendo

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi, Isihaka Mchinjita amesema anatarajia kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Tanzania Bara. Kwa sasa nafasi hiyo kwa upande wa Tanzania Bara inashikiliwa na Doroth Semi ambaye ameitumikia kwa kiwango cha kuridhisha. Mchinjita, ametangaza nia hiyo mkoani Lindi ambapo ameweka wazi baada ya…

Read More