Kiongozi wa upinzani aliyechomwa kisu shingoni Korea Kusini ahamishwa hospitali
KIONGOZI wa chama cha upinzani cha Democratic Party cha Korea Kusini, Lee Jae-myung amewahishwa hospitali mjini Seoul baada ya kuchomwa kisu shingoni na mtu asiyejulikana. Shambulio lilitokea wakati Lee alikuwa akikagua eneo lililopendekezwa kufanyika ujenzi wa uwanja wa ndege mpya huko Busan. Mshambuliaji aliyevalia taji la karatasi lenye maandishi “Mimi ni Lee Jae-myung,” kwanza alikaribia…