WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YATUMIA MAONESHO YA NANE NANE KUPUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI,KUTOA ELIMU YA KISHERIA
Na Asha Mwakyonde, DODOMA KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali kupunguza migogoro ya kisheria miongoni mwa wananchi, Wizara ya Katiba na Sheria inaendelea kutoa huduma katika maonesho ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea kitaifa jijini Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, ametoa pongezi kwa Wizara hiyo baada ya kutembelea banda lao Agosti 6, 2025,…

