RC KUNENGE AIPONGEZA DAWASA, AWAPA JUKUMU MADIWANI
Na Mwandishi Wetu,Pwani MKUU wa Mkoa wa Pwani (RC), Mheshiwa Abubakar Kunenge amesema ushirikishwaji wananchi kwenye miradi ya maendeleo unaofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ni wa mfano na unapaswa kuigwa na taasisi zingine. Aidha, amewaomba Madiwani kutoa ushirikiano kwa DAWASA ili kuhakikisha wananchi wanatunza vyanzo vya maji…

