MRADI WA TAZA KUFUNGUA SOKO JIPYA LA BIASHARA YA UMEME AFRIKA.
Na Mwandishi Wetu,Mbeya Imeelezwa kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Zambia kupitia Tunduma (TAZA) umefikia asilimia 83.45 huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Mei 2026 na hivyo kufungua soko jipya la biashara ya umeme barani Afrika. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo…

