Nyuma ya pazia mtumishi wa umma aliyefukuzwa kazi Benki

  • Uchunguzi umebaini alitenda makosa lukuki ya kiutumishi yaliyosababisha kufukuzwa kazi
  • Mojawapo ni la kua mtu na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani
  • Atumia magazeti kumchafua mwajiri wake na taasisi aliyokuwa akiifanyia kazi

Na Mwandishi Wetu

YAMEMKUTA. Ndivyo unavyoweza kusema namna mmoja wa mtumishi wa benki moja maarufu inayotoa mikopo kwa wakulima nchini kufukuzwa kazi na kuanza kuichafua benki hiyo katika baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijàmii huku akiwa amefukuzwa kazi muda mrefu sasa.

Baada kusambaa taarifa hizi, Taifa Tanzania ilijaribu kupata ukweli wa sakata hilo na kubaini kuwa mtu huyo alikuwa mtumishi wa Taasisi hiyo na kwa sasa amefutwa kazi kutokana na makosa ya kiutumishi aliyoyatenda na taratibu zote za kisheria zimefuatwa.

Hata hivyo alikata rufaa na kushindwa katika maeneo yote ya kisheria ambayo inamtaka mtumishu ambaye hakuridhika na hukumu aliyopewa.

Inaelezwa kuwa aliyekuwa mtumishi wa Taasisi hiyo alifukuzwa kazi kutokana na makosa aliyotenda wakati akiwa kazini na wala haikutokana madai aliyotoa kuwa alifukuzwa kazi akiwa likizo ya uzazi.

Inaelezwa Mei 13, 2022 akiwa dereva wa taasisi hiyo alimgonga mtu na kumuua katika kijiji cha Mganza barabara ya Nguruka-Kigoma na kufunguliwa kesi ya usalama barabarani namba 6/2022 katika Mahakama ya Wilaya ya Kigoma, alihukukiwa kwenda gerezani mwaka mmoja kwa kosa hilo la jinai au kulipa faini ya shilingi elfu hamsini. Ambapo alichagua kulipa faini na kuwa huru.

Hukumu hiyo ilitolewa tarehe 18/07/2022 na Hakimu K.M.Matembei ambaye ndiye Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Kigoma.

” Kimsingi haipo hivyo, huyo dada amefanya makosa mengi akiwa kazini ambayo yamepelekea yeye kufukuzwa na ni muda mrefu sana sasa saivi anatafuta huruma ya wananchi kwa kutumia vyombo vya habari” kilisema moja ya chanzo chetu cha habari.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini muhusika amefanya makosa mengi ya kukiuka sheria za utumishi wa umma lakini kwa sasa yanashindwa kuwekwa wazi kwa sababu bado yapo kwenye ngazi za juu za sheria.

Hii inatokana na yeye kushindwa kwa hoja kutokana na kujua ukweli halisi kutokana na makosa yake aliyoyatenda ya ukiukwaji wa sheria na taratibu aliyoyafanya kuwa wazi.

Jitihada za kuutafuta uongozi wa Benki hiyo ulifanikiwa lakini walikataa kuzungumzia chochote katika sakata hili huku wakitusihi kuwa wavumilivu kusubiri maamuzi ya kisheria yaliyopo ngazi za juu kuhusu swala hili.

Taifa Tanzania linaahidi kuendelea na awamu ya pili ya stori hii kuonyesha ukweli wa makosa yenyewe ambayo muhusika anayaficha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *