Na Ibrahim Yassin,Songwe
WANANCHI wa vijiji vya Lupeta , Mwalisi na Lema wameishukuru serikali inayoongozwa na Rais Dkt,Samia kupitia Serikali chini ya Shirika la Taifa la Madini STAMICO kwa kurahisisha mawasiliano na kuwanusurua na vifo vitakanavyo na ajali za kusombwa na maji mto Mwalisi.
Daraja la mto Mwalisi ni moja ya Daraja hatari mkoani humo lililosababisha kuwepo kwa hatari mbalimbali ikiwemo watu kuliwa na mambo huku wajawazito wakijifungulia njiani wakishindwa kuvuka hasa nyakati za mvua za masika.
Serikali za awamu zote ziliahidi kujenga Daraja kubwa bila mafanikio huku wananchi wakiendelea kuhatarisha Maisha yao kwa kuvuka kwenye kivuko cha mianzi kilichosababisha baadhi kutumbukia na kuliwa na mamba miaka ya nyuma.
Baada ya kukamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha Wilaya za Rungwe na Kyela Mkoa Mbeya na Wilaya ya Ileje,Mbozi Mkoani Songwe,wananchi wametoa ya moyoni wakipongeza serikali kwa kusikia kilio kilichodumu tangu nchi hii ipate uhuru.
Wakizungumza mwishoni mwa wiki wananchi hao wamesema kukamilika kwa daraja hilo kutarahisisha pia usafiri na usafirishaji wa mazao kutoka shambani lakini wanafunzi kuvuka kwa urahisi kwende shuleni ukilinganisha na ilivyokuwa awali.
Peter Maa mratibu wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira Kaburo akiwa na mkandarasi anayejenga daraja hilo William Shija wakitoa maelezo kwa mwandishi wa habari hizi eneo la tukio.
Uswege Kabuje mwenyekiti wa Kijiji cha Kapeta,amesema miaka ya nyuma watu kadhaa walikufa maji wakati wanavuka Daraja la mianzi kufuata huduma upende wa pili,kukamilika kwa Daraja wanauhakika wa kuongezeka Uchumi kwani shughuri za kilimo zinapatikana upande wa pili.
‘’Changamoto ya ukosefu wa Daraja ulidumu tangu nchi ipate uhuru lakini kwa utawala wa Dkt,Samia mambo yametimia,anauhakika wananchi wataongeza nguvu kwenye kilimo kwani Daraja lipo na hata usafiri wa bodaboda na guta utakuja kubeba mazao’’amesema Kabuje.
Peter Maa ni Mratibu wa mgodi wa makaa ya Mawe Kiwila Kabulo amesema daraja hilo limepunguza gharama za uzalishaji wa makaa ya mawe katika Mgodi wa Kiwira wakati huo kwani watalazimika kutumia kilometa 14 kutoka eneo la machimbo Kwenda mgodini na kurudi.
Amesema awali walitumia njia ya mzunguko ya kilometa zaidi ya 70 kwenda na kurudi kupitia wilaya ya Kyela huku Maroli yakibeba tripu 3 kwa siku lakini kwa sasa watatumia kilometa 7 kwenda na kurudi kilometa 7 wakiwa na uhakika wa kubeba tripu zaidi ya 10 kwa siku.
William Shija ni mkandarasi anaye jenga daraja hilo amesema limeshamilikia kwa asilimia 98 kilichobaki ni kufungua sehemu ya njia kusawazisha kifusi ili lianze kutumika na kuwataka wananchi kulinda miundombinu hiyo.