Na Mwandishi Wetu
‘’Uwepo wa soko la Pamoja chanzo kupaa uchumi,wachimbaji wadogo wakichangia asilimia 51 pato la Taifa,utoroshwaji madini haupo Rais Dkt,Samia anapaswa kupongezwa’’
WANUNUZI wa madini ya dhahabu mkoani Songwe,wamempongeza Rais Dkt,Samia Suruhu kwa kufanya mapinduzi ya kiuchumi katika sekta hioyo,iliyopelekea kupaa mara dufu kimapato ukilinganisha na miaka ya nyuma..anaripoti Ibrahim Yaasin,Songwe.
Wakizungumza leo Juni 19/2024 katika ofisi za madini zilizopo Mkwajuni wilayani Songwe,mkurugenzi wa kampuni ya ununuzi wa madini Mohammed Sharif amesema tangu Rais Dkt,Samia aingie madarakani ameibadirisha sekta ya madini na kufanikiwa kudhibiti utoroshwaji wa madini.
Amesema awali walikuwa wakiwafuata wachimaji majumbani mwao kuomba wawauzie dhahabu huku wengine wakigoma wakitaka kusafirisha nje ya mkoa hali hiyo iliwapa ugumu kpata mzigo na kuhatarisha usalama wao na fedha zao kwani ulinzi ulikuwa mdogo.
Amesema baada ya ujenzi wa soko la Pamoja na kuweka bei elekezi kwenye mbao za matangazo,wame weza kununua dhahabu kiurahisi na hata wachimbaji wamekuwa akipeleka kuuza hapo hali iliyomaliza utoroshwaji wa dhahabu.
Ameongeza kuwa Pamoja na kupata mafanikio hayo,wameweza kusaidia jamii inayozunguka soko hilo,katika ujenzi wa sekta za afya,elimu,umeme,miundombinu ya barabara na kusaidia ujenzi wa nyumba za ibada ikiwemo misikiti.
Mbali na kusaidia jamii kwenye ujenzi,Sharif amesema pia wameweza kuwajengea nyumba 2 wazee wasiojiweza ambazo zipo asilimia 80 za ujenzi Pamoja na kutoa michango mbalimbali halmashauri na kwenye jamii.
Nae Said Mabruki mnunuzi wa madini (DIRA) amesema kupitia mafanikio hayo wameweza kutoa ajira Zaidi ya 60 katika kada mbalimbali kwa vijana wanaojishughurisha na uchimbaji kwa kuwapa mitaji.
Fove Swaleh mnunuzi wa madini,amesema siku za hivi karibuni Rais Dkt,Samia kupitia Waziri wa madini Anthony Mavunde,alitoa vitalu 19 kwa vikundi vya wachimbaji hali itakayowasaidia kukopesheka kwa kuwa watakuwa na leseni ambazo ni mdamana wao.
Chonde Malembo amesema miaka hii mitatu ya Rais Dkt,Samia Suruhu hali ya kipato kimeongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma,kwani madini yote yanauzwa kwa bei elekezi ambayo kwa gram 1 Tsh,176,000 na wanunuzi wote wapo sehemu moja serikali inachukua mapato kiurahisi,hakuna utoroshwaji wa madini na hadi kufikia mwezi Mei walikusanya asilimia 71 za mapato..