Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
KITUO Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema mwaka wa fedha wa 2024/25 wananchi wasitegemee maendeleo makubwa au miradi mipya kwakuwa kwakiasi kikubwa fedha zimeelekezwa zaidi katika matumizi ya kawaida na kulipana mishahara.
Kauli ya LHRC imetolewa wakati wabunge wakijadili bajeti ya Sh Trilioni 49.35 iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba ambapo katika fedha hizo mapato ya ndani (Serikali Kuu) ni Sh Trilioni 33.25,mapato ya halmashauri ni Sh Trilioni 1.35,misaada na mikopo nafuu kutoka Washirika wa Maendeleo ni Sh Trilioni 5.13 huku mkopo ya Kibiashara Ndani na Nje Sh Trilioni 9.6.
Akizungumza wakati akifanya uchambuzi wa bajeti hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Wakili Fulgence Massawe alisema bajeti imekuwa ni ya matumizi ya kawaida zaidi kuliko maendeleo hivyo ni ngumu kuanzisha miradi ya maendeleo kupitia bajeti hiyo.
‘Ukiangalia bajeti yetu 70% ni matumizi ya kawaidana 30% ndio ya maendeleo,hii inaonyesha tusitegemee maendeleo makubwa au miradi mipya ya maendeleo kwani bajeti yetu ni ya matumizi ya kawaida na kulipana misharaha na madeni.
‘Matumuzi mengine ya kawaida yamekuwa ni ya anasa ambayo ni pamoja na magari ya kifahari na watendaji wakuu wa nchi kuishi Dar es Salaam muda mwingi kuliko Dodoma inayopelekea kuhudumia miji mikuu miwili ambapo ni gharamakubwa,‘alisema Wakili Massawe.
Alisema pia kuna haja ya kuangalia ukubwa wa serikali.kuongeza cheo cha Naibu Waziri Mkuu kinaongeza gharama kwa serikali.
‘Wizara zimekuwa nyingi na nyingi kwa sasa zina manaibu waziri na naibu katibu hata kwa wizara huko nyuma hazikuwana manaibu,bajeti yetu mara nyingi imekuwa na nakisi lakini nakisi ya bajeti haiathiri matumizi ya kawaida.Kunapokuwa nakisi kinachoathirika ni miradi ya maendeleo na si matumzi yakawaida. Kuna haja ya serikali kujiangaliza kwenye hili na kuelekeza mapato mengi kwenye maendeleo ya nchi,‘alisema Wakili Massawe.
Alisema LHRC wanaamini kuwa maendeleo ni msingi wa haki za binadamu pia.
Akizungumzia kuhusu vyanzo vya mapato alisema vyanzo vimendelea kuwa vile vile na wanaochangia bajeti kwa njia ya kodi ni wananchi wachache.
Alisema hata vyanzo vingine vya mapato kama vilevi sio endelevu kwani watanzania wakiamua kubadilisha mfumo wa maisha na kuacha kunywa nakuvuta ina maana nchi itashindwa kujiendeleza.
‘ Kuna haja yaserikali kubani vyanzo vipya vya mapato. Mfano mchango wa halmshauri kwenye bajeti yetu ni mdogo sana,halmashuri nazo zimeshindwa kubuni vyanzo vipya mfano kupima ardhi kwawingi na kumilikisha wananchi ili kupata kodi ya ardhi.
‘Madini hayajawa na mchango mdogo kwenye bajeti yetu mbali na Tanzania kuonekana tuko nafasi ya tatu Afrika kwa kuchimbana kuuza dhahabu na tanzanite inapatikana Tanzania pekee.madini haya hayajawa na msaada mkubwa kwenye mchango wa mapato,
‘alisema Wakili Massawe.
Akizungumzia kuhusu fedha za kigeni alisema kumekuwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni nchini na serikali imeshindwa kutambua chanzo cha uhaba huu kwakuwa imeonekana tumeona serikali inapiga marufuku matumizi ya fedha za kigenikitu ambacho kitaharamisha matumizi hayo na hali kuwa mbaya zaidi kwakuwa zina uhitaji mkubwa kwenye wan chi
‘Kinachosababisha uhaba wa pesa za kigeni ni uwiano kati yabidhaa tunazouza nje na tunazoingiza. Serikali inatakiwa kuwana mkakati wa kufufua na kuhamasisha uzalishaji wa mazao yabiashara kama kahawa, pamba, mkonge, korosho nk.
‘Serikali lazima iwe na mkakati ya kujenga mazingira rafiki na kuhamasisha wawekezaji wakubwa kuja kuwekeza nchini kwetu,ukiangalia ukanda huu mbali na Tanzania kuwa na rasilimali nyingi bado Tanzania haijawahi kuwa chaguo nambamoja la uwekezaji,‘alisema.
Alisema mazingira yanayokwamisha uwekezajiTanzania yanajulikana na serikali imeyavumbia bia kuchukuahatua stahiki.