Vijana 150 wapatiwa elimu ya uzalishaji wa mbogamboga kutoka shirika la SAIPRO Same

Na Mwandishi Wetu

Vijana 150 Kutoka katika Kata 12 wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wamepatiwa elimu ya uzalishaji wa mboga mboga lengo likiwa ni kujikwamua kiuchumi Kutoka shirika lisilokuwa la kiserikali la Saipro.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa shirika hilo la Saipro Mwadhini Myanza wakati akizungumza kwenye maonyesho ya mbegu mbalimbali za mboga mboga kupitia mradi wa world vegetable center chini ya ufadhili wa shirika la USAID wilayani Same Mkoani Kilimanjaro maonyesho yaliyoenda sambamba na maadhimisho ya sikukuu ya sabasaba.

Amesema kwakutambua thamani ya mlaji wameona uzalishaji wa mboga mboga kupitia mbegu za asili ni fursa kubwa kwa vijana kutumia nafasi hiyo katika kujiajiri.
“Tumefanya hivi kwalengo mahususi kabisa kwaajili ya kuifikia jamii hasa walaji na mradi huu umekuja chini ya ufadhili wa shirika la USAIDna mradi huu tumelenga kuwafikia watu zaidi ya 300 kwenye maeneo mbalimbali wilayani Same”.
“Alisema mwenyekiti wa saipro”

Kwaupande wake afisa maendeleo ya jamii Kutoka saipro Winifrida nichombe amesema kupitia mradi huo wa uzalishaji wa mboga mboga kwakutumia mbegu za asili kutaongeza kipato kwa kundi kubwa la vijana ambao watakuwa mstari wa mbele katika kuchangamkia fursa hiyo.

Akizungumza katika tukio hilo katibu tawala wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Upendo Wella pamoja na kuwapongeza shirika hilo la Saipro pia akasema wao kama serikali wataendelea kusimamia na kufuatilia matokeo ya kile ambacho shirika hilo limenuia kwa wananchi.

Wella amesema mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanamchango mkubwa sana katika maendeleo ya jamii hivyo wao kama serikali wataendelea kusimamia na kufuatilia matokeo ya malengo kusudiwa kwa jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *