MADEREVA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHALI NA KEMIKALI YA SODIAM SIANIDI

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

WANANCHI wamesisitizwa kutokimbilia magari ya mizigo yanayopata ajali kwakuwa mengi yanabeba kemikali ikiwemo ya sodiamu sianidi ambayo ina madhara makubwa kwa binadamu.

Akizungumza  katika uzinduzi wa kampeni ya kuelimisha kuhusu  kemikali ya sodiamu sianidi kwa wananchi  wanaoishi pembezoni mwa barabara  ya mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya karibu,Meneja wa Afya ,Usalama na Mazingira wa kampuni ya Freight Forwaded Sadiki Yusufu amesema  kemikali hiyo ambayo ni bora kwa uchimbaji wa madini duniani ina madhara makubwa endapo ikiamwagika na kuingia maji.

“Kemikali ya sodiamu sianidi pamoja na kutumika katika masuala mengine yakimaabara nchini lakini asilimia 90 ya kemikali inatumika katika kuchimba madini,kemikali ina uwezo mkubwa wakulainisha dhahabu,ili ifike migodini uwa inasafirishwa sasa lengo la kutoa elimu hii ni kuwaelimisha wananchi hasa wanaotumia vyombo vya usafirishaji wasigusane na haya magari maana endapo gari litaanguka na kumwagika ikishika maji inaleta madhara kwa binadamu,”amesema Yusufu.

Amesema kemikali hiyo ambayo imeingia Tanzania mwanzoni mwa miaka 1990 inaweza kuondoa dhahabu kutoka kwenye mwamba kwa ubora zaidi kushinda mercury ambayo inasifika muda mrefu kwa kufanya shughuli hizo.

Amesema tangu iingie nchini imekuwa ikitumika kwa uangalifu na kwamba haijawahi kusababisha ajali ya aina yoyote iliyogharimu maisha ya watu.

Naye Mkemia Dereck Masako akizungumza kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa  Serikali kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) amesema zoezi  la shughuli  ya elimu ya ufahamu kuhusu kemikakali ya sodium sianaidi. 

“Sianidi inatumika katika kuchenjulia,tunajua dhahabu ina thamani lakini upatikanaje wake unatumia kemikali mbalimbali,kemikali hii ina uwezo wakulainisha dhahabu ukiiweka inapotea kama sukari  ukiiweka kwenye maji,kwa hiyo ni kali  sana elimu hii itasaidia wananchi wasipate madhara hasa kipindi chakusafirishwa,”amesema Mkemia Masako.

Amesema kampeni hiyo ni mahususi kwa ajili ya watu wanaoishi pembezoni mwa barabara kuanzia Dar es Salaam mpaka mikoa mingine.

“Tunatoa elimu hii kwa  sababu kemikali hii ina madhara makubwa ikichanganyika na  mqji inaweza kusababisha kifo,”amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *