Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu, amewatakawadau wa Kemikali kuzingatia matumizi salama na sahihiya kemikali ili kuchochea maendeleo katika nchi yetukwani kemikali ikitumika vizuri kwa kuzingatia miongozoina faida kubwa tofauti na pale inapotumika vibaya.
Dkt. Jingu amesema hayo leo Desemba 11,2024 wakati akifungua mafunzoya siku tatu ya usimamizi na udhibiti wa kemikali nabidhaa zake kwa wasimamizi wa kemikali yaliyoandaliwana Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikalikupitia Ofisi ya Kanda ya Mashariki na kufanyika jijini Dodoma.
“Shughuli za kiuchumi na maisha ya kila siku yamwanadamu, zinategemea uwepo wa kemikali, mafunzohaya yana tija kubwa sana kwa sababu yatatusaidia kuwana matumizi salama na sahihi ya kemikali, hivyoyatachochea maendeleo kwa sababu kemikali ina faida kubwa pale tu inapotumika vizuri, lakini ikitumika vibayamadhara yake ni makubwa sana mfano Vifo na athari za kiafya na mazingira” alisema Dkt. Jingu.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu ameipongezaMamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kaulimbiu ya mafunzo hayo inayosema “Mafunzoyanaendelea” kwani elimu haina mwisho na kwenyeNyanja ya kemikali mambo mengi yanaibuka kila siku hivyo elimu ndio silaha kuu ya kuwezesha matumizisalama na sahihi ya kemikali kwa lengo la kulinda afya za binadamu na mazingira ambayo kemikali hizo hutumika.
Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amesema Mamlaka ya Maabara ya MkemiaMkuu wa Serikali inaendelea kutimiza majukumu yake yakisheria ikiwemo kutoa elimu na kufanya usajili na ukaguziwa kemikali ili kuiwezesha Serikali kufahamu ni kemikaliipi imeingizwa na nani kwa ajili ya matumizi gani na je inaruhusiwa kisheria ili kulinda afya na mazingira.
“Hadi kufikia jana Desemba 10, 2024 jumla ya wadau 5933 wanaojihusisha na kemikali wamesajiliwa rasmi baada yajitihada za Mamlaka ambapo ukirejea mwaka 2012 wakatiutekelezaji wa Sheria ya usimamizi na udhibititi wakemikali za viwandani na majumbani sura ya 182 unaanzajumla ya wadau 12 tu walisajiliwa rasmi” alisema Dkt. Mafumiko.
Berina Valence na Jimmy Mkongwe ni washiriki waMafunzo hayo wamesema wamepata elimu kubwaambayo itawasaidia kuondokana na usimamizi wamazoea wa kemikali kwenye maeneo yao ya kazi kwani nihatari kwa afya za wafanyakazi na mazingira
“Mafunzo haya yana tija kubwa sana kwa sababu kunabaadhi ya mambo tumezoea kufanya kimazoea lakinihapa tunapata shule inayotuamsha na kuturudishakwenye muelekeo sahihi” walimaliza.