Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
CHAMA Cha Wafanyakazi wa Viwanda,Biashara,Taasisi za Fedha Huduma na Ushauri (TUICO) kimewataka wanachama wake kujipanga katika kugombea na kuchagua viongozi wa wa chama hicho watakaolinda uhai maslahi ya chama.
Kauli hiyo imetolewa leo Februari 10, 2025 Mwenyekiti wa TUICO Paul Sangeze wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa hali Bora kati ya TUICO na mwajiro na TUICO na chama Cha wafanyakazi,alisema wanachama wa chama hicho wanategemea kufanya uchaguzi ndani ya mwaka huu ambapo wametakiwa kuacha kupitisha viongozi bila kupingwa kwakuwa uchaguzi wa aina hiyo hauleti viongozi wazuri.

“Mwaka huu 2025 ni mwaka wa uchaguzi wa chama chetu cha TUICO,ninawaomba kila mmoja wetu katika nafasi yake kuhakikisha chama kinapata viongozi bora watakaolinda uhai wa chama.
“Hakikisheni kuwa kanuni,masharti na utaratibu wa chama unafuatwa kusiwe na kupitisha kaa viongozi bila kupingwa hata kama mgombea ni mmoja utaratibu wa kura ufuatwe yaani kuwa na Ndiyo au Hapana kila mmoja asisahau kumwamba Mwenyezi Mungu tuwezw kuvuka salama,”amesema Sangeze.

Amesema pia ni wajibu wa kila mmoja na watendaji wote wa chama kuhakikisha wanakilinda chama dhidi ya maadui wasiokitakia mema chama.
Akizungumza kuhusu mafanikio amesema katika kipindi cha mwaka mmoja chama kimeweza kupata wachama wapya 15,032,kufunga mikataba ya hali bora 98.
Amesema migogoro 303 ilipokelewa ambapo kati ya hiyo na migogoro 214 ilishinda huku kamati 108 za majadiliano ziliundwa.

Amesema ziara 3166 zilifanyika ,mikutano 44,854 uliofanyika ,semina 44,150 huku wafanyakazi bora 182 walipata zawadi.
