
DCEA YAMNASA KINARA MIRUNGI,YATEKETEZA EKARI 285.5
Na Mwandishi Wetu,Same MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, imefanya operesheni maalum wilayani Same, mkoani Kilimanjaro kuanzia Machi 19 hadi 25 mwaka 2025. Katika operesheni hiyo, ekari 285.5 za mashamba ya mirungi zimeteketezwa na watuhumiwa saba (7) wamekamatwa, akiwemo kinara wa biashara haramu ya…