NaAMwandishi Wetud,Dar es Salaam
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya upimaji wa mtihani wa kidato cha nne huku takwimu ikionesha ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.26 ya wasichana wote ambapo kati ya watahiniwa 526,620 waliofanya mtihani huo wasichana 278,108 ambao ni watahiniwa wa shule wamefaulu kwakupata daraja la kwanza mpaka la nne.
Akizungumza jijini Dar es Salaa.a matokeo hayo, ya mtihani uliofanyika Novemba 17, 2025, Januari 31, 2026 jijini Dar es Salaam. Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed, amesema jumla ya watahiniwa 595,810 walisajiliwa kufanya mtihani huo, wakiwemo wasichana 318,910 sawa na asilimia 53.53 na wavulana 276,900 sawa na asilimia 46.47.
Alisema kati ya watahiniwa hao jumla ya wataniniwa 526,620 sawa na asilimia 94.98 ya watahiniwa wa shule wenye matokeo wamefaulu kwakupata daraja la kwanza mpaka la nne kwa mwaka jana wakati mwaka 2024 watahiniwa waliofaulu walikuwa 477,262 sawa na asilimia 92.37 hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.61.

“Kati ya watahiniwa 526,620 waliofaulu,wasichana nk 278,108 sawa na asilimia 94.26 ya wasichana wote wenye matokeo na wavulana 248,512 sawa na asilimia asilimia 95.79 ya wavulana wote wenye matokeo,”alisema Profesa Said.
Alisema watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 16,794 sawa na asilimia 73.83 kwa mwaka jana wakati mwaka 2024 watahiniwa wakujitegemea walikuwa 15,703 sawa na asilimia 62.51 ya waliofaulu mtihani huo hivyo ufaulu wa watahiniwa umeongezeka kwa asilimia 11.32 ukilinganisha na ufaulu wa mwaoa 2024.
Akizungumzia kuhusu matokeo ya jumla Profesa Said alisema ufaulu wa wanafunzi umeendelea kuimarika na umefikia asilimia 94.98, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.61 ikilinganishwa na mwaka uliuliopita.
Alisema jumla ya watahiniwa 526,620 wamefaulu kwa kupata madaraja ya I, II, III na IV, huku ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu ukiwa ni wanafunzi 255,404 sawa na asilimia 46.1, idadi ambayo imeongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Profesa Mohamed ameeleza kuwa jumla ya wanafunzi 569,883 walifanya mtihani huo wakiwa wamesajiliwa katika shule 5,864, huku watahiniwa wa kujitegemea wakiwa 25,927 waliosajiliwa katika vituo 813 nchini.
Aidha , NECTA imesema jumla ya wanafunzi 77 wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika kuandika lugha ya matusi kwenye skripti za mitihani na wengine kujihusisha na udanganyifu, ambapo kati yao 47 walitoka katika vituo vya mtihani na 30 kutoka shule mbalimbali.


