Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imesema jumla ya meli 112 zenye tani 3,874,055 za sulphur zimeingia nchini tangu mwaka 2021 ambapo sheria ya kuingiza kemikali hiyo ilipoanza kufanya kazi.
Akizungumza jijink Dar es Salaam leo Julai.24, 2026 wakati wakufungua kikao cha waingizaji,wahifadhi na wasafirishaji wa kemikali aina sulphur kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko,Mkurugenzi wa Huduma ya Udhibiti Daniel Ndiyo alisema kemikali hiyo inaingizwa nchini na kusafirishwa kwenda nchi za Jamhuri ya Demokrasi ya Congo na Zambia.

Alisema kemikali aina sulphur inatumika katika nchi hizo kwa ajilinya utengenezaji wa Copper hali hiyo imesababisha Tanzania kupitisha mzigo mkubwa wa sulphur.
“Miaka ya nyuma mzigo wa namna hii ulikuwa hauruhusiwi kuingia nchini lakini mwaka 2019 Bunge ilibadilisha sheria ikaruhusu,2020 zikatungwa kanuni kuanzia Julai 2021 tukaanza kuingiza sulphur.
“Tangu kipindi hicho jumla ya meli 112 zimeingizwa tani 3874,055 kwa wastani meli moja inaweza kuingiza mpaka Sh Bilioni moja,biashara hii kwa sasa inatuingiza fedha pamoja na kwamba ilikuwa hairuhusiwi,ukipiga mahesabu ya tani ya sulphur moja inabeba malori 100 ambayo wananchi wanapata ajira,”alisema Ndiyo.

Alisema mpaka sasa kuna wasafirishaji wa sulphur 212 wanaotambulika na kwamba kwa muda wa miaka miwili jumla ya ajali 62 zilitokana na sulphur zimerekodiwa katika malori zaidi ya 100
Alisema hivyo kutokana na ukubwa wa biashara hiyo GCLA kwakushirikiana wasafirishaji wanaangalia namna ya kuweka njia bora za usafirishaji kwa utaratibu mzuri na usalama.

“Tunataka kuangalia namna tunaweza kuboresha usafirishaji wa sulphur inaingia nchini si kwa matumizi ya nchini ni ya nchi za nje,sulphur ni mzigo ambao unachangia kuingiza kipato kwa bandari ya Dar es Salaam na Tanga,GCLA tuliweka taratibu za upakuaji na tahadhali ili isije kuwaka moto kwakuwa sifa ya sulphur ni kuwaka moto lakini sasa tunataka kuona njia bora zaidi za usafirishaji,”alisema Ndiyo.
Alisema kikao hicho kitajadili matakwa ya sheria na kanuni pamoja na kuziboresha na kuhakikisha wanatimiza matakwa ya kanuni kwakuwa biashara hiyo ina faida kubwa .
“Wakienda na sulphur wanarudi na copper kwa hiyo bandari yetu inatoa mzigo,tunataka kujadili changamoto pamoja na kuboresha na kuendeleza biashara hiyo,hakuna kitu ambacho kimenyooka lazima kiwekwe sawa,”alisema.
Naye mwakilishi wa kampuni yaDSM Corridor Group Limited Mhandisi George Alando alisema kama kampuni wamekuwa wakufanya mafunzo mbalimbali kwa madereva yakuhifadhi sulphur.
“Unahifadhi sulphur na kuifanyia packaging baada ya hapo zinasafirsihwa kwemda Zambia na DRC,tunafuata muongozo uliotolewa na ofisi ya mkemia na tunaandaa tararibu zetu kama ofisi,” alisema.
Alisema pamoja na tahadhali hizo bado kuna changamoto za uelewa wa jamii kuhusu sulphur utakuta na kwamba inapofanyika operesheni wananchi wanaiona kama sumu na kwamba hawaelewi wakati gani inakuwa sumu wakati gani inakuwa kawaida .

