RAIS DK.SAMIA MGENI RASMI BARAZA LA EID

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Eid linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kati ya Machi 31 au Februari Mosi kulingana na kuandamana kwa mwezi.

Akizungumza leo Machi 28 mwaka 2025,kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislam (Bakwata) na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir,Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Omar amesema Baraza hilo la litatanguliwa na swala ya Eid itakayofanyika katika msikiti wa Mfalme wa VI makao makuu ya Bakwata jijini Dar es Salaam.

“Baada ya mwezi wa Ramadhan kinachofuata Eid,kwa niaba ya baraza Kuu la Waislam  natangaza tutaswalia Eid kitaifa Dar es Salaam,swala itafanyika katika msikiti wa mfalme wa Sita.

“Baraza litafanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere,mgeni rasmi tunategemea atakuwa rais Dk.Samia na amesema atashiriki kuanzia asubuhi mpaka jioni kwenye Baraza la Eid,”amesema Sheikh Walid.

Amesema  Bakwata inawaalika waislam kushiriki katika siku hiyo muhimu kwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *