NIDA kufungia matumizi vitambulisho vilivyotelekezwa Serikali za Mitaa

Na Aziza Masoud, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetangaza kufungia matumizi ya namba za utambulisho vya Taifa (NINs) kuanzia Mei Mosi mwaka huu kwa watu wote ambao wametumiwa ujumbe wa kuwataka kuchukua vitambulisho hivyo na hawajatekeleza.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam leo Aprili 14, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa NIDA James Kani alisema uamuzi imetolewa kufuatia maelekezo yali yotolewa Januari 21 mwaka huu ambapo mamlaka ilitangaza kuanza kwa zoezi maalum la kukusanya vyote vya Taifa vilivyokuwa katika ofisi za kata, vijiji, mitaa, vitingoji na shehia na kuvirejesha makao makuu.

“Mtakumbuka zoezi hili lilienda sambamba na utumaji ujumbe mfupi wa simu(sms) kwa wale walikuwa hawajachukua vitambulisho vyao na kuwataka wafike kuvichukua ndani ya siku thelathini tangu wanapopata sms vinginevyo tunafungia matumizi ya namba zao za utambulisho hivyo kushindwa kupata huduma.

“Kwakuzingatia kuwa tulishatuma sms karibu kwa watu wote ambao vitambulisho vyao vilikusanywa katika maeneo husika na kwa kuwa tulishawatangazia kwamba tutafunga namba za matumizi ya NIN kwa wale wote ambao tumekwisha zalisha vitambulisho vyao na kuwapekea ujumbe wa kuvifuata lakini bila sababu yoyote ile ya msingi hawakujitokeza kuvichukua nawajulisha rasmi kuwa kuanzia Mei Mosi mwaka huu tunafungia namba zao mpaka watakapojitokeza kuchukua vitambulisho vyao, “amesema Kaji.

Amesema dhamira yao na Serikali kwa ujumla ni kuona kila kitambulisho kilichotengenezwa kinachukuliwa na muhusika na hasa ukizingatia vimeigharimu serikali fedha nyingi.

Amesema tangu kuanza kwa zoezi lakukusanya vitambulisho hadi kufikia Machi 23 mwaka huu jumla ya wananchi 1,880,608 sawa na asilimia 157 ya watu wote waliokuwa hawajachukua vitambulisho vyao
wametumiwa ujumbe mfupi na kuupokea.

“Itakumbukwa kuwa wakati tunavikusanya vitambulisho hivyo kutoka ofisi za kata, vijiji na mitaa tulikuwa na vitambulisho 1,200,000 vilivyokuwa havijachukuliwa na wahusika, hii Ina maana kwamba takribani watu wote waliokuwa hawajachukua vitambulisho vyao walikwisha pata ujumbe huo mfupi wa simu ya mkononi.

“Ziada ya ujumbe 680,608 zilitumwa inayofanya jumla ya jumbe fupi zilizokwishatumwa kuwa 1,880,608 kwa waombaji wapya waliosajiliwa kwa kipindi hili na ambao vitambulisho vyao vimechapishwa tayari,” amesema Kaji.

Amesema kwa mujibu wa takwimu hizo idadi ya watu waliojitokeza kuchukua vitambulisho maana ya kupata ujumbe no 565,876 sawa na asilimia 30 tu ya watu wote waliotumiwa na kupokea ujumbe.
Mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *