GREEN ACRES,CRDB  WATOA MSAADA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA MWANANYAMALA

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

SHULE za Green Acres  imefanya ziara na kutoa msaada wa vitu mbalimbali  kwa ajili yakuwasaidia wagonjwa  waliojifungua,wenye watoto njiti  na waliolazwa kwa sababu mbalimbali katika wodi ya watoto  hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.

Msaada huo ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 25 tangu kaunzishwa kwa shule hizo mwaka 2000.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa Shule za Green Acres,Jacklyne Rushaigo alisema shule hizo kama wametembelea na kutoa msaada kwa hospitali hiyo kama sehemu ya kurudisha kwa jamii kutokana kutoa huduma ya elimu kwa jamii ya Watanzania kwa muda mrefu.

“Kama taasisi ya elimu inayojali maadili, utu na huduma kwa jamii, tumetembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hizo,”amesema Rushaigo.

Amesema ziara hiyo imelenga kuwafariji watoto waliolazwa kwa kuwapatia sadaka pamoja na ujumbe wa matumaini na upendo kutoka kwa wanafunzi wetu.

Katika ziara hiyo waliambatana na mdhamini mkuu wa sherehe za Maadhimisho ya shule benkiya CRDB ambayo imekuwa kinara katika kutambua na kujali vijana katika sekta ya elimu,ambapo Meneja wa benki hiyo Kanda ya Pwani Badru Idd  alisema ushiriki wao katika maadhimisho ya Green Acres ni muhimu kwakuwa benki hiyo pia inafikisha miaka 30 mwaka huu.

“CRDB tumeungana na Green Acres kuja hapa Mwananyama kutoa mkono wa asante  kwa wateja na jamii ambayo tunaifanyoa kazi,”amesema Idd.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *