EQUITY YAWAKUTANISHA WAWEKEZAJI 236 KUTOKA NCHI 15

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

WAWEKEZAJI 236 kutoka nchi 15 za  Tanzania,Ulaya,,nchi ya Falme za Kiarabu pamoja na  Marekani wamekutana nchini kwa lengo la kujadili jinsi ya kukuza biashara zao na kufanya uwekezaji  nchini Tanzania ili kuweza kupanua wigo wa masoko ya wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.

Wawekezaji hao kwa pamoja wanakutanishwa na Benki ya Equity   kwa lengo la kuongeza thamani za biashara ili kufanya uchumi wa nchi zao kuimarika na kuvutia wawekezaji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Leo Mei 19, 2025 kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Dk.Selemani Jafo,Mkuu   WA Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),Profesa Tandi Lwoga  aliipongeza benki ya Equity kuwa kiunganishi wa wawekezaji hao na wafanyabiashara kusaidia kuwakutanisha kwa pamoja na kuona  upatikanaji wa masoko na mikopo ili kuwasaidia katika  bidhaa mbalimbali wanazoziwekeza.

“Equity imefanya kazi kubwa ambayo ilianza tangu  mwaka 2022 na imekuwa ni Jukwaa  nzuri la kuwakutanisha  wafanyabiashara wa ndani na nje,hii ni fursa ya kuongeza uwekezaji nchini ambapo wanaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan  katika kuvutia uwekezaji na kuwekeza Tanzania.

”Ni fursa kubwa ambayo Tanzania imeipata kupitia Equity Bank kwaajiliya kuweza kuwaleta wawekezaji na kuja kuwekeza katika sekta tofauti tofauti ikiwemo ya Kilimo,Utalii,Usafirishaji ,Ujenzi na Seta nyingine zote zitakazoenda kuchangia kuinua uchumi nchi,”alisema.

Alipongeza juhudi za benki ya  Equity kwa kuwaleta wafanyabiashara na wawekezaji pamoja na kuzitaka taasisi nyingine nchini za umma na binafsi kuwa kiunganishi kwa wafanyabiashara mbalimbali  ili kuvutia wawekezaji zaidi kwani Tanznaia inafursa nyingi kuanzia Utalii,Kilimo,Huduma,Mawasiliano na Teknolojia.

Kwa Upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania, Isabella Maganga alisema  Jukwaa lao linalofahamika kwa jina la ‘Trade Mision’ ni maonesho ya kibiashara ambayo yanawakutanisha wafanyabiashara wa sekta mbalimbali kulingana na mahitaji ya soko,mazingira ya kiuchumi na fursa zilizopo.

Alisema wafanyabiashara waliowakutanisha katika jukwaa hilo ni takribani 53 kutoka katika nchi 15 za Afrika na wengine nchi ya Ulaya,Marekani na Nchi za Uarabuni na USA  huku wafanyabiashara wa kitanzania wapo wafanyabiashara 183.

”Lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara hao ni kukuza fursa za wafanyabiashara wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania ili kuyakuza masoko yao na kuongeza thamani biashara zao na kuchukua bidhaa kupeleka nje ,tunataka kukuza biashara za nje  na kufanya uchumi unakuwa na kuvutiwa wawekezaji,”alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Biashara ,Viwanda na Kilimo(TCCIA),Oscar Kissanga,alisema chemba yao imewapeleka  wafanyabiashara waliopo katika Chama chao ambao wapo katika sekta ya viwanda,bianshara na Afya ili waweze kukutana na wenzao kutoka nchi mbalimbali ikiwemo ya Kenya na Uganda ili kufanya mashirikiano ya biashara wanazofanya,kubadilishana fursa na kutafuta masoko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *