JAB YAWATAHADHALISHA WALIOPANGA KUWASILISHA VYETI FEKI KUJISAJILI

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB),Tido Mhando ametangaza rasmi kuanza kwa usajili wa waandishi wa habari katika mfumo wa TAI-Habari huku akiwaonya wasiokuwa wanataaluma lakini wamo kwenye tasnia waliojipanga kughushi vyeti ambavyo si halali wakati wa kujaza taarifa zao.

Mhando ametangaza tahadhali hiyo leo Mei 19, 2025 wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari katika Ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mtaa wa Jamhuri Jijini Dar es Salaam,alisema maombi ya ithibati na vitambulisho (Press Cards)yatafanyika kupitia mfumo unaoitwa TAI-Habari,hatua inayolenga kuboresha huduma,kuimarisha usimamizi wa taaluma ya uandishi wa habari na kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho kwa waandishi waliothibitishwa.

”Waandishi wanapaswa kuingia kwenye kiunganishi https;/www.taihabari.jab.go.tz na kufuata maelekezo ya kujisajili,baada ya kujaza taarifa kwa usahihi,mwimbaji atapokea msimbo(code)kupitia SMS na kiungo kwenye barua pepe ili kuendelea na hatua za kujaza wasifu,kufanya maombi,kupata ankara ya malipo,kulipia na kuwasilisha maombi ya kupata kitambulisho(Press Card),”alisema.

Alisemaa viambatanishi vinavyohitajika wakati wakuomba ithibati na kitambulisho ni pamoja na namba ya simu na barua pepe vinavyofanya kazi,picha ndogo iliyoskaniwa,vyeti vya elimu vilivyoskaniwa kwa mfumo wa PDF na kuthibitishwa na Mamlaka husika na TCU kama vyuo vya Kati vithibitishwe na NACTVET,barua ya utambulisho kutoka taasisi anayotoka utambulisho kutoka taasisi anayotoka au anakopeleka kazi zake ikiwe ni mwandishi wa kujitengemea,nakala ya Kitambulisho cha Taifa  pamoja na ada ya ithibati Sh.50000 ada itakayodumu ndani ya miaka miwili.

Mhando alisema watu wanapaswa kuomba ithibati na kupewa vitambulisho ni pamoja na Wahariri,waandishi wa habari walio katika vyombo rasmi,Waandishi wa habari wa Kujitegemee,wapiga picha ,wazalishaji wa habari na watangazaji wa redio na televisheni wanaofanya kazi katika vyombo vya habari.

Alisema kwa mujibu wa kanuni ya 17 (2) wote waliotajwa kupata nafasi ya kuomba ithibati hizo wanapaswa kuwa na kiwango cha elimu ya kuanzia Stashahada ya masuala hayo au Shahada ya fani nyingine yoyote na Shahada ya Uandishi wa Habari.

“Kumekuwepo na taarifa zinazodokeza kuwepo kwa baadhi ya watu wanaojaribu kuwasilisha vyeti vya kughushi au nyaraka zisizo halali kwa lengo la kujipatia usajili a vitambulisho ni kinyume na taratibu.

”Jambo hili sio tu kikuka maadili ya taaluma ya habari bali ia ni makosa ya jinai yanayoadhibiwa kwa mujibu wa sheria ya nchi,”alisema.

Aliwatahadhariasha waandishi wa habari watakaobainika kuwasilisha vyeti au nyaraka za kughushi watachukuliwa hatua kali bila kujali hatua waliokuwa wamefikia katika mchakato wa usajili.

”Hatua hizi zitajumuisha kufutiwa mara moja usajili wao,kuwasilishwa katika vyombo vua sheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki pamoja na kupigwa marufuku kujihusisha na shughuli za uandishi wa habari au majukwaa mengine ya kitaaluma,”alisema.

Alisisitiza mfumo wa TAI HABARI umeanzishwa kwa nia njema ya kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari kwa misingi ya uwajibikaji,weledi na heshima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *