COOP BENKI ITACHOCHEA UPATIKANAJI WA RASILIMALI FEDHA

Na Asha Mwakyonde, DODOMA

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Ushirika Tanzania (Coop Bank), Godfrey Ng’urah, amesema kuwa kuanzishwa kwa benki hiyo ni jitihada za makusudi za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuchagiza maendeleo na mchango wa sekta ya kilimo katika Pato la Taifa ikiwamo kuhakikisha sekta hiyo inakua kwa asilimia 10 kufikia mwaka 2030.

Hayo aliyasema juzi bungeni mara baada ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akiwasilisha hotuba ya Wizara hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/2026, alisema wamejionea maendeleo makubwa katika bajeti ya mwaka 2024/2025 kumekuwa na matokeo chanya yakiwamo uanzishwaji wa benki ya ushirika Coop Bank.

Alisema katika serikali ya awamu ya sita nchi  imeendelea kujionea mgawanyo wa kutosha kwa wakulima ambapo sekta ya kilimo ikikua wa asilimia hizo mwaka 2030.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa sekta ya kilimo itakuwa ikichangia angalau asilimia 30 hadi 40 ya Pato la Taifa ikilinganishwa na sasa ambapo asilimia 65 ya Watanzania katika sekta hiyo wanachangia asilimia 16 hadi 20.

“Uwiano huu  hauko sawa lazima tuwe na jitihada za makusudi asilimia 65 ya watu kuchangia asilimia 16 hadi 20 kuna hitajika jitihada za makusudi kuongeza uzalishaji kwenye patao la Taifa, bajeti imejikita katika kuhakikisha sekta ya uzalishaji miundombinu ya uzalishaji mbegu,mbolea, dawa,pembejeo, soko kwa wakulima walio wengi wanapata fedha, mgawanyo sahihi wa  rasilimali kupitia bajeti ya kilimo ili kuongeza uzalishaji kwa asilimia kubwa kwa Watanzania walio wengi,” alisema.

Alieleza kuwa uwepo wa benki hiyo kutachochea upatikanaji wa rasilimali fedha za kutumia fursa za miundombinu huku akisema kuwa na mbegu, mabwawa,dawa  hakutoshi lazima kuwe na mitaji ili wakulima waweze kupata mbegu bora, dawa na pembejeo kwa lengo la kuyafikia masoko.

Ng’urah aliongeza kuwa benki hiyo ni ya kimkakati kwa kushirikaiana na benki nyingine ikiwamo benki ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),kuhakikisha wanakuwa na mitaji katika soko la kilimo.

Aliongeza kuwa kwa miaka mingi mgawanyo wa rasilimali fedha kwenda kwenye kilimo ni chini ya asilimia 10 huku akifafanua kwamba mwaka jana kulikuwa na mtawanyo wa rasilimali fedha kwenye wa trilioni 37. 5 kati ya fedha hizo ambazo zilitolewa na benki zote nchini ni asilimia 10 ndio iliyoenda katika sekta ya kilimo.

Alisema kuwa sekta ya kilimo ndio yenye watu wengi na kwamba uwepo wa benki hiyo ni kutaka kutanua wigo wa  kuhakikisha mgawanyo wa fedha hizo katika mitaji na  shughuli za  kilimo  zinaongezeka kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2030.

“Tumedhamiria kuongeza ujumuishi wa kifedha , mgawanyo wa fedha kwenye uchumi Kwa sasa angalau asilimia 38 ipo kwa watu binafisi , watumishi na wafanyabiashara hivyo benki hii tabadilisha takwimu hizi ifikapo mwaka 2030 tukiwnza na bajeti ya mwaka huu kuhakikisha Watanzania walio wengi wanapata huduma za kibenki,” alisema.

Aliongeza kuwa benki hiyo ni kipekee ambayo itakuwa na bidhaa na huduma zilizotengenezwa Kwa muktadha wa sekta yenyewe kuvutia watu wengi.

Ng’urah alisema benki hiyo imejikita kuhakikisha wanapunguza gharama za mitaji katika kilimo.

“Katika hotoba ya Waziri Bashe alisema serikali imewekeza fedha kama dhamana, kuna dawati dhidi ya vijana na wanawake kuja kwenye kilimo itajayodhaminiwa na wadau wa maendeleo katika dawati maalum kwenye benki ya ushirika,” alisema.

Alisema kuwa wanatarajia kuwa na bidhaa mahusus za kibenki ambazo zinaweza kumudu uchumi wa vijana ambao wanaanzisha shughuli za kilimo kwa mara ya kwanza.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alieleza kuwa nj matarajiao yao uwepo wa benki hiyo kuanzia mwaka huu hadi ifikapo mwaka 2030 watachagiza uchumi jumuishi wa kifedha kutoka asilimia 22 na kufikia asilimia 50 kwa kuwafikia Watanzania wasiopungua milioni 10.

Alifafanua kuwa kwa sasa Watanzania waotumia huduma za kibenki ni milioni 5 huku akisema ni dhamira ya benki ya ushirika kwa sababu inalenga wakulima vijijini wanawake, vijana pamoja na Watanzania walio wengi kwenye shughuli za kilimo biashara.

Alifafanua kuwa benki hiyo SI ya kilimo pekee bali kuna mnyororo wa thamani katika kilimo biashara, usafirishaji, pembejeo, wajasriamali na wale wanaofuata bidhaa nje ya nchi na kuzileta nchini.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa benki ya Coop itasaidia kuongeza shughuli za kibiashara za wajasriamali katika mnyororo wa thamani kilimo biashara.

Alisema Moja ya changamoto katika vyama vya ushirika ni ukosefu wa mitaji huku akifafanua asilimia kubwa ya wakulima wanakopeshwa mazao yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *