NMB KUHUDUMIA ZAIDI YA WATEJA 900,000 SABASABA

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

ZAIDI ya wafanyabiashara 3000 na wateja 900,000 wanatarajiwa kutembelea banda la benki ya NMB katika Maonesho ya 49 ya  Biashara Dar es Salaam (DITF)   maarufu kama Sabasaba kwa ajili yakupata huduma mbalimbali ikiwemo kufungua akaunti.

Akizungumza leo Juni 30, 2030 katika  viwanja vya Sabasaba,Mkuu wa Matawi na Mauzo wa benki ya NMB Donatus Richard amesema wapo katika maonesho hayo kwa ajili yakutoa huduma mbalimbali ikiwemo kufungua akaunti kuanzia za watoto mpaka za wazee ambapo tumesambaza mawakala kila kona ya viwanja hivi kwa ajili ya kutuma na kutoa fedha.

“Lengo letu ni kuwahudumia zaidi wafanyabiashara 3000 ambai wapo kwenye maonesho haya lakkni pia tunatarajia kupokea wateja  zaidi ya 900,000 ambao tunatawatarajiwa kutembelea ndani ya viwanja hivi,”alisema Richard.

Alisema wapo kwa ajili ya  kuwahudumia wafanyabiashara na wateja ambao wamekuja kwenye  maonesho hayo hivyo wafanyabiashara ambao wnafika katika maonesho  ambao hawana akaunti wanaweza kuwahudumia.

Alisema pia benki imefungua dirisha lakulipa malipo yote ya serikali kama ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)  na malipo mengine.

Alisema kama kauli mbiyu ya mwaka huu NMBkama benki wanaendelea kuwa karibu na wateja wao kwakutoa huduma mbalimbali

“Kwa msimu wote wa Sabasaba watakuwepo pia watalaam wetu wa mikopo na kuna wafanyakazi wanahitaji mikopo hapa ukija tutakuelekeza namna yakuomba mkopo kwakutumia benki yako ya NMB,”alisema.

“Tuna watalaam wa kilimo na watalaam mbalimbali wa fedha,kwenye maonesho haya tumekuja  mara nyingi sasa hivi tumekuja kivingine,”alisema Richard.

Akizungumzia kuhusu mikopo ya kilimo alisema wameendelea kutoa elimu inayohusiana na masuala na sasa wana akaunti maalum kwa ajili ya wakulima na kutoa mikopo yenye masharti nafuu na inayotoka kwa haraka.