TAASISI ZA FEDHA ZATAKIWA KUFUATA NYAYO ZA TCB KATIKA UWEKEZAJI

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
SERIKALI imesema uchumi Tanzania una kiwango kikubwa cha sekta isiyo rasmi hivyo imezitaka taasisi za fedha kuhakikisha zinafanya ubunifu wakuongeza fursa za uwekezaji unaotokana na wajasiriamali.

Akizungumza jana wakati wa akizinduzi wa Hatifungani ya Stawi Bondi ya Benki ya Biashara Tanzania (TCB) yenye thamani ya Sh Bilioni 150, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya,alisema bado uchumi wa Tanzania una kiwango kikubwa cha sekta isiyo rasmi wengi wa wajasiriamali wengine wamesajiliwa lakini hawaendi kwa njia ambayo itawafanya wawe rasmi lakini wengine wengi hawajasajiliwa kabisa.

“Kundi hilo linahitaji tiba ili wale wajasiriamali waweze kukua wawe wajasiriamali wakubwa kwa sababu ule uwezo wakuwa mjasiriamali ndani ya jamii yetu ni muhimu kwa ajili ya kukidhi matakwa ya bidhaa za huduma katika jamii.

“Lakini pia uchumi wetu una haja ya kukuza sekta binafsi kwa sababu bado ni mdogo bado ni changa ipo haja yakuikuza ili iweze kukua na kuwa kampuni kubwa badae,uzoefu wetu hata hao wanashiriki wanashiriki kwakiwango kidogo ambapo ili waweze kushiriki zaidi.”alsiema Mwandumbya.

Alisema wajasiriamali ili waonekane wanashiriki katika uchumi wanapaswa waende kwenye miradi ya serikali na inayotoa fursa kwenye shughuli ama fursa mbalimbali zakiuchumi ambayo inapaswa kukua na kuweza kutoa mchango katika uchumi.

Akizungumzia kuhusu hatifungani ya stawi alisema benki hiyo itaongeza uwezo wake wakutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu katika kundi ambalo limelengwa na hivyo kuhakikisha kwamba wajasiriamali wanapata mikopo nafuu itakayowawezesha kustawi.

“Uzinduzi wa stawi wa bondi wa benki ya TCB ni hatua muhimu inayounga mkono dhamira ya kupitia masoko ya mitaji mjini,ni chombo chakifedha chakuwekeza na ni njia yakuimarisha ushiriki wa wananchi katika uwekezaji wa kitaifa,kupunguza utegemezi wa mikopo yakigeni na kuongeza mapato ya serikali,”alisema Mwandumbya.

Alisema ili kuweza kufikia malengo hayo wizara ya fedha imeona ifanye hatua mbalimbali ikiwemo kusimamia sera zakifedha ambazo zinalenga zaidi kuongeza ushirikishwaji wakifedha na kukuza uchumi shirikishi.

“Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zakifedha kuhakikisha kama hizi zinaendelea kuanzishwa na kufanikisha dira ya Taifa ya ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu,wizara ya fedha ina dhamana yakusimamia sera za fedha na uchumi.

“Moja ya malengo makuu ya sera hizo ni kupunguza utegemezi wa mikopo ya gharama kubwa kutoka nje,kuimarisha ushiriki wa wananchi katika kusimamia maendeleo ya nchi yao kupitia uwekezaji wa ndani ,”alisema.

Awali akizungumza kuhusu hatifungani hiyo Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa TCB,Adam Mihayo alisema Hatifungani hiyo ya Stawi Bondi ni ya miaka mitano itakuwa na gharama ya Sh Bilioni 150 ambapo utaratibu wa uwekezaji utafanyika kwa awamu tatu.


Alisema Stawi Bondi inatoa riba ya asilimia 13.5 kwa wawekezaji, ambayo inalipwa kila baada ya miezi mitatu.

“Faida itakayopatikana kutokana na hatifungani hii itaelekezwa katika kuhakikisha wajasiriamali wadogo na wa kati wanapata mikopo nafuu itakayowawezesha kustawi.
“Stawi Bond ni zaidi ya chombo cha kifedha, ni uthibitisho wa dhamira ya TCB katika ajenda ya uchumi wa Tanzania,kwa kuwawezesha wajasiriamali na kurahisisha upatikanaji wa mikopo nafuu, tunahakikisha kuwa masoko ya mitaji yanaongeza thamani kwa wahusika halisi wa uchumi wwetu.alisema Mihayo.

Alisema uzinduzi huo unakuja wakati ambapo soko la mitaji la Tanzania linashuhudia ukuaji mkubwa.

“Hadi Juni 27, 2025, Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) limefikia mtaji wa jumla wa Shilingi Bilioni 19,481.40 za Kitanzania, ambao umechochewa kwa kiasi kikubwa na utendaji mzuri wa sekta za benki na viwanda.

“Kuanzishwa kwa Mahakama ya Masoko ya Mitaji na sheria za Soko la Hisa la Dar es Salaam zilizofanyiwa marekebisho 2025 kumeimarisha uadilifu wa soko, ukwasi, uwazi na ufanisi,”alisema Mihayo.

Alisema hiyo metengeneza mazingira wezeshi kwauwekezaji wa hatifungani kama vile Stawi.

“Soko la dhamana leo ni mojawapo ya njia salama zaidi kwa wawekezaji, inayotoa mapato thabiti na fursa ya kuchangia ustawi wa uchumi wa taifa, na uhimilivu wa kifedha wa muda mrefu nchini.”alisema Mihayo.

Alisema kwa sasa benki ya TCB inapita katika safari ya mageuzi inayoongozwa na Mpango Mkakati wake wa 2024-2028, unaoangazia mabadiliko ya mizania, uwekaji upya wa chapa, matumizi ya teknolojia ya kidijitali, udhibiti wa hatari na usimamizi wa rasilimali watu.

” Benki inapanua wigo wa utoaji huduma wake na kuwafikia wateja wapya hasa wajasiriamali wadogo na wa kati. Hatua hii inaenda sambamba na ubunifu wa bidhaa na huduma za kidijitali ikiwemo TCB Popote, Internet banking, na malipo ya QR,”alisema Mihayo.