Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewakumbusha wateja wake kutumia nishati safi yakupikia kwakutumia vifaa vya umeme vinavyotumia umeme nafuu katika msimu huu wa sikukuu.
Kupitia video iliyotolewa na Tanesco inayoonyesha wananchi wakifurahia matumizi ya nishati safi ya umeme kwa kupikia kwakutumia vyombo mbalimbali vya umeme ikiwemo majiko ya umeme ambayo yanatumia umeme mdogo.
“Tanesco inakukumbusha msimu huu wa sikukuu, usipate tabu kuandaa chakula cha familia nyumbani,pika kwa umeme nishati safi na salama,utaokoa muda jikoni,utalinda afya yako pia ni gharama nafuu,”ulisema ujumbe huo.
Vyakula vyote vya sikukuu unaweza kuvipika kwa chini ya unit 1 tu ya umeme ambayo ni sawa na Sh 356 tu hivyo watumiaji wa umeme watumie jikoni kwa furaha nyumbani.


