WANANCHI MAKURUMLA WALALAMIKIA SHIDA YA MAJI

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

WANANCHI   wa kata ya Makurumla wamelalamikia shida ya maji  yanayosambazwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) ambapo wanadai kuwa eneo hilo hakuna maji na hata ikitokea yametoka yanakuwa machafu.

Wakizungumza kwa nyakati katika kikao maalum cha halmashauri kuu ya eneo hilo Job Mwakajumba ambaye anaishi katika  mtaa wa Jongo  kata ya Makurumula alisema kuwa wanakabiliwa  na chagamoto ya maji na imekuwa kero kwa kata hiyo mtaa kwa Jongo

Alisema katika kukabiliana na changamoto hiyo kulichimbwa kisima katika mtaa huo lakini maji yalitoka siku moja hayajawahi kutoka tena.

“Wananchi tumekuwa tukilalamika sana kuhusu maji mtaa wa pili wa Kagera umekuwa ukipata maji,jambo hili limekuwa kero kwetu  hakuna maji lakinj  tunaambiwa Ruvu Maji yamejaa mvua zinanyesha lakini maji hakuna ,”alisema Mwakajumba.

Alisema tatizo la shida ya maji  Dawasa wanalijua vizuri na wananchi wamekuwa wakishangaa chagamoto hii inatoka wapi.

“Dawasa waache siasa kwenye maisha ya watu,wanapaswa  kubadilika kwani wananchi wanahitaji maji na sio maneno ,”alisema Mwakajumba.

Naye mwananchi mwingine Liberata Mduga  naye alisema wamepokea ilani ya kata ya makurumula lakini chagamoto yao  kubwa ni maji toka walivyopata maji mwaka jana mpaka leo hayajatoka tena.

“Tunashaangaa bado wanakuja kusoma mita na tumejaribu kufatilia lakini wamekuwa wakisema kunachagamoto chagamoto,”alisema Mduga.

Alisema kumekuwa na mgao wa maji ambao wamekuwa wakitarajia kuupata wamekuwa hawaupati hivyo wamemuomba Waziri wa Maji Juma Aweso na idara ya maji kuwaona wananchi hao kwasababu wanateseka hasa wanawake kwakuwa wanabeba maji kutoka mbali na wanatumia gharama kubwa.

“Ndoo ya maji gharama ya chini ni Shilingi mia tano  mpaka Shilingi elfu moja,hao wanauza ndo tunashangaa wanayatoa wapi wakati katika mabomba ya eneo hilo maji hayatoki,uwa wanatuuzia na maji ya chumvi na siku nyingine ya bomba,”alisema Mduga.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya makurumula Bakari Kimwanga leo tumekutana katika kikao Cha Halmshauri kuu maalumu ambapo tumewasilisha taarifa ya kazi ya utekelezaji wa ilani ambayo imeagazia maeneo yote muhimu ikiwemo Sekta ya afya.

Akizungumzia kuhusu suala la maji alisema anategemea Dawasa watafanya utekelezaji waliokubaliana ambao utakwenda kuhakikisha  unarudisha tabasamu kwa wananchi hasa eneo la kata ya Makurumla.

“Naamini kwa juhudi zinazofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Maji Juma Aweso  na Meneja wa Dawasa Magomeni watakwenda kushirikiana pamoja azma ya Rais Dkt Samia inakwenda kutekelezwa na kuondoa chagamoto ya maji katika eneo hili,”alisema Kimwanga.

Akizungumzia wizi wa maji alisema watu hao wamekuwa wakitumia mfumo wanaoiita nyoka lakini wanaendelea kushirikiana na Dawasa kutatua chagamoto na kufanikiwa kuwakamata wahusika wanaofanya hivyo na kupigwa faini .

Alisema katika eneo hilo kati ya nyumba zote nyumba moja tu ndo imekuwa ikipata maji jambo ambalo limekuwa ni la kushagaza.

Akizungumzia kuhusu miundombinu alisema kata hiyo imekamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha Makulumla ambacho kinafanya vizuri na mpaka mwezi ulioisha kimefunga na idadi ya kinamama 82 ambao wamejifungua Kwa njia ya kawaida na operation.

Alisema hayo ni Mapinduzi makubwa awali ilikuwa ni wakinamama wawili ndio wanajifungua kwa mwezi .

“Katika sekta ya miundombinu mbinu na barabara za ndani ambapo mkakati wa Halmashauri hiyo ya Ubungo Kwa mwaka wa fedha ujao ni kujenga barabara za ndani Mitaa,”alisema Kimwanga.

Kwa upande wa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ubungo, Henry Mwenge alisema suala la maji ni suala lenye mustakabali wa maisha ya Kila mtu kwani maji ni uhai .

“Hatuna njia nyingine ya kupata maji hivyo mwananchi anavyokosa maji anakumbana na chagamoto, katika utoaji wa maji Dawasa inapaswa kutoa taarifa za ukweli Kwa wananchi Ili kuondoa sitofahamu na kuweka uwazi zaidi ,”alisema Mwenge.