MASOKO YA MADINI YAIMARISHA UWAZI KUDHIBITI UTOROSHAJI
Na Mwandishi Wetu,Dodoma Tume ya Madini imesema kuanzishwa kwa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini nchini kumeongeza uwazi katika biashara ya madini na kusaidia kudhibiti utoroshaji wa rasilimali hiyo, hatua iliyochangia kuongezeka kwa mapato ya Serikali. Akizungumza leo katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali jijini…

