MFUMO WA KUSAJILI WAANDISHI WA HABARI KIDIGITI KUZINDULIWA APRILI MWISHONI

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

WIZARA ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Habari (Maelezo) kwa kushirikiana na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imesema uzinduzi wa mfumo wa kidigiti wa usajili wa waandishi habari unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Aprili ama mwanzo wa mwezi Mei, 2025.

Taarifa iliyotolewa leo Machi 28 mwaka 2025 na  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya  waandishi Patrick Kipangula imeeleza kuwa baada ya kupokea maoni ya wadau mbalimbali yanayolenga kuimarisha zaidi usalama, ubora, ufanisi na wenye kukidhi mahitaji.

“Tameamua kuongeza muda wa ukamilishaji wa mfumo wa usajili wa kidigiti hadi mwishoni mwa mwezi wa Aprili 2025,hivyo uzinduzi wa mfumo huu utafanyika mwisho wa mwezi Aprili au mwanzo wa mwezi Mei, 2025,”amesema Kipangula.

Hata hivyo amesema  kazi ya ukamilishaji wa mfumo wa kidigiti wa usajili wa waandishi wa habari inaendelea kwa mafanikio makubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *