ENVAITA ILIVYOFANYA MAPINDUZI YA KIDIGITALI

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam 

JAMII imetakiwa kubadilika na kuacha kutumia njia za kizamani zakualika   watu  katika matukio mbalimbali  badala yake watumie njia zakidigitali ili kuokoa muda na kupunguza usumbufu.

Akizungumza leo Aprili 28, 2025  Meneja wa Mawasiliano wa Envaita Praygod Mushi amesema utumiaji wa mialiko ya kadi kwa njia ya kidigitali unaokoa mambo mengi japokuwa watu  hawana imani nazo.

“Njia ya kidigitali ni nzuri lakini  changamoto iliyopo watu bado hawaelewi wanadhani ni utapeli,pia kumekuwa na  mtazamo mtu akitumiwa kadi za mialiko kwa njia ya simu anaona amedharaulika, lakini ndiyo njia sahihi na inayofaa katika kipindi hiki cha utandawazi wakidigitali,”amesema  Mushi.

Amesema mialiko ya kidigitali pia inasaidia kupanga bajeti kwakuwa unakuwa na idadi kamili ya watu wanaohudhulia tukio lako.

Akizungumzia kuhusu kampuni ya Envaita ambayo imekuwa ikitoa huduma za kutoa mialiko kidigitali amesema huduma hiyo ni gharama nafuu na rahisi kufikika.

“Mialiko yakidigitali yote inatumwa kwa njia ya Whatsapp uwe na smart ama huna unapata mwaliko wako,Kwa wale wasiokuwa na simuza smart wanatumiwa kwenye simu ndogo namba zao za kadi na taarifa zao zote zinakuwa mtandaoni.

“Pia kuna watu unaweza ukamtumia mwaliko labda asielewe na akahisi kuwa ni utapeli sisi  uwa tunapiga simu kuwapa taarifa ili wasiwe na wasiwasi,siku ya sherehe pia tunahudhulia kwa ajili ya kuscan kadi,”amesema Mushi.

Amesema kadi haiwezi kutumika mara mbili Wala hakuna atayeweza kuingia kwenye sherehe bila kualikwa.

Amesema baada ya shughuli kampuni inatuma ujumbe mfupi wakuwashukuru watu ambao inatoka kwenye familia.Kampuni hiyo ambayo imeanza kutoa huduma hizo mwaka 2022 imejjimarisha katika mikoa zaidi ya kumi na imeshagawa ajira za kudumu zaidi ya 30,.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *