Na Mwandishi Wetu,Dar es Sala
WAZIRI wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameiagiza bodi mpya ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kulisimamia shirika hilo lijiendeshe kwa weledi na liweze kutoa huduma bora.
Mbarawa ameyasema hayo baada ya kuzindua bodi mpya ya ATCL ambapo Mwenyekiti Mweyekiti wake ni Prof. Neema Mori.

“Mbarawa amasema kuwa pamoja na mafanikio mengine,ATCL imeweza kufungua na kufanya safari katika vituo 26, Atcl inaendelea kusafirisha mizigo kwa kutukia ndege maalum ya mizigo aina ya B767-300F yenye uwezo wa kubeba tani 54“,Alisema Mbarawa
Aidha Mbarawa amegiza kwa bodi hiyo kuhakikisha kuwepo na ratiba za kuaminika, bei nafuu ya ushindani, ubunifu na teknolojia ,upanuzi na mtandao wa safari mikataba na ushirikiano,upanuzi wa mtandao wa Safari mikataba na ushirikiano kujiunga na Mashiriks mengine, usimamizi bora wa rasilimali, kampeni za masoko pamoja kuweka mazingira mazuri ya sera.

Mwenyekiti wa Bodi wa ATCL Prof. Neema Mori amesema watahakikisha wanafanya kazi kwa weledi ili shirika hilo liweze kuwa na tija kwa nchi.
Huku Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Peter Ulanga amesema mpaka sasa shirika hilo lina jumla ya ndege 16 hivyo Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Anga.

