UVCCM KUCHAGUA WABUNGE NA WAWAKILISHI KUNDI LA VIJANA LEO

Na Asha Mwakyonde, DODOMA

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Taifa leo unafanya Mkutano Mkuu Maalum wakuchagua wabunge kundi la vijana na wawakilishi wa kundi hilo kupitia Jumuiya ya UVCCM.

Mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe 438 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao watapiga kura katika Mkutano Mkuu Maalum.

Hayo yalisemwa jana jijini hapa na
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Taifa, Jessica Mshama alisema wanaimini na vijana hao watakachaguliwa na kwamba watakuwa wawakilishi wao wazuri kutetea maslahi ya vijana nchini.

Alisema vijana watakaopata nafasi ya kuchaguliwa watawatumikia vema vijana nchini kwa kuwa wamepikwa na kuiva vizuri na Chama cha Mapinduzi ambacho kina nguvu.

“Mkutano huu utakuwa wa kihistoria maandalizi na yanaheshimisha Jumuiya yetu pamoja na Chama na kumuheshimisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo anaifanya na kutetea maslahi ya vijana nchini,” alisema.