Na Asha Mwakyonde, DODOMA
BENKI ya Ushirika (COOP BANK), kesho inasaini mkataba wa udhamini watakaoshirikiana na
Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF), ambao umewapatia zaidi ya bilioni 8. 5 fedha zitakazotumika kama dhamana kuwapatia vijana wa Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Build a Better Tomorrow- BBT),fedha kutoka katika maeneo atamizi.
Hayo aliyasema jana jijini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Godfrey Ng’ura wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la benki hiyo lilipo kwenye Jiji Cha Ushirika katika maonesho ya wakulima maarufu Nane nane alisema lengo ni kuwawezesha vijana hao kuyafikia masoko.
Alisema kuwa fedha hizo kwa kuwa vijana hao hawana dhamana na miundombinu sahihi wameshirikiana na AGITF
kupata dhamana ili kuwasaidia vijana kupata mikopo.
Alieleza kuwa wanatambua maono ya vijana katika siku za usoni huku akisema ni lazima waweze kujenga kesho iliyobora kupitia BBT.

Aidha aliongeza kuwa wanatambua wasomi wengi wanajiari katika kilimo huku akisema serikali inawekeza ambapo kibajeti ambapo mwaka hadi mwaka inaongeza bajeti katika sekta ya kilimo ambayo imeongeza trilioni 1.2.
“Benki inashiriki katika maonesho haya ya nane nane mwaka 2025 kama miongoni mwa wadhamini wakuu wa maonesho haya benki hii ni namba moja na mdau wa kilimo,” alisema.
Alisema kuwa soko lao mama katika masoko kisekta ni kilimo na kwamba wamiliki wa benki hiyo zaidi ya asilimia 51 ni wakulima ambapo wanavyama Vikuu vya kilimo katika mazao yote ya kimkakati na kwamba mfumo wao wa masoko na mauzo ya mazao ya kilimo inasimamiwa na sekta ya Ushirika.
Ng’ura aliongeza kuwa mazao yote ya kahawa,korosho,chai, mbaazi na ufuta huku akisema mfumo wa kukusanya na kuuza nje ya nchi unasimamiwa na vyama Vikuu vya msingi AMCOS …pamoja na wakulima mmoja mmoja ambao ni wanachama na wamiliki wa benki ya Ushirika Tanzania.
Aidha aliwaalika wananchi na wanaushirika na wadau wa mnyororo mzima wa kilimo, wakulima vijana na wadau wote kutembelea banda hilo.
Alifafanua kuwa benki hiyo imepeleka bidhaa muhimu inayotambulika kwa jina la Ghala Pesa ambayo itazinduliwa mwaka huu sio kwa wanaushirika bali mnyororo mzima wa biashara ambayo itawaruhusu wakulima kupata kutumia mazao yao ghalani kama dhamana na kupata malipo kabla hawajauza.
