NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
MATARAJIO ya Serikali katika kuinua sekta ya Sanaa, Ubunifu kupitia Haki Miliki Tanzania (COSOTA) huenda yakaingia majaribuni baada ya Mkurugenzi wake Mteule Loy Mhando kutokuwa tayari kwenda kufanyakazi katika eneo hilo.
Mjumbe huyo wa Bodi alieleza wasiwasi wake kwa sharti la kutotajwa jina na kueleza kuwa hivi karibuni Waziri wa Habari, Sanaa karibuni na Profesa Paramagamba Kabudi alimteua Loy ambaye awali alikuwa Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu kutoka Wakala wa Usajili wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Amesema kuwa pamoja na kupata Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa COSOTA, lakini kuna kila dalili kugomea hatua ya kwenda kuingoza ofisi hiyo.
“Tumekuwa na mipango kadhaa hasa kupitia COSOTA katika kusimamia haki miliki na ubunifu, Loy ni mmoja kati ya watu muhimu ambaye tuliposikia uteuzi wake binafsi nilifurahi sana na kuona sasa tumepata mtu sahihi.
“Lakini cha ajabu hadi sasa hajaripoti kazini na hatujui kwa nini, ila tunaamini kwa mipango yetu ni wazi tumepata mtu sahihi ambaye anaendana na kasi ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, hasa katika kusimimia haki miliki, mirabaha kwa sekta za miliki na sanaa hapa nchini. Tunaamini tutaungana naye tuje kwa pamoja kusimamia mkakati wa Serikali yetu.
“Rais alionyesha nia ya kuboresha mazingira ya wasanii kwa kutambua mchango wa sanaa katika Taifa letu na umuhimu wa kazi zao, na pia kutafuta njia za ziada za kukuza kipato chao pamoja na uchumi, tumefikia hatua muhimu ambapo COSOTA imefikia makubaliano ya Ushirikiano na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhusu suala la kulipia leseni (mirabaha) kwa matumizi ya muziki katika viwanja vya ndege.
“Makubaliano haya, ambayo ni sehemu ya Mkataba kati ya TAA na COSOTA, yatasaidia wasanii wa muziki wanapata haki yao ya malipo kutokana na matumizi ya muziki katika maeneo ya viwanja vya ndege nchini,” amesema Mjumbe huyo wa Bodi ambaye hakutaka kutanjwa jina lake
Amesema hiyo ni hatua kubwa katika kuhakikisha kuwa wasanii wanapata masoko ya kazi zao, na kupata mapato kutokana na vyanzo mbalimbali vya kazi zao, na kwamba haki zao zinaheshimiwa kikamilifu.
Aidha ameongeza kuwa katika kipindi cha Septemba 2023 hadi Novemba 2024, COSOTA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilikusanya zaidi ya Shilingi bilioni 1.1
Hata hivyo alipotafutwa Loy na kuulizwa kuhusu mikakati yake kuhusu COSOTA kama Afisa Mtendaji Mkuu mpya alisema bado hajawa tayari kuzungumzia mikakati yake ya kazi katika nafasi yake hiyo mpya.
Akizungumzalia suala hilo, Loy amesema hajawa tayari kuzungumzia lolote na akiwa tayari ataeleza.
“Sijawa official kuzungumza chochote kuhusu hilo pindi nikiwa tayari nitakueleza tu,” amesema. Loy.
Ikumbukwe kuwa mwandishi wa habari alitaka kufahamu mikakati yake na jinsi atakavyoweza wasaidia wasanii katika kusimamia mirabaha na haki zao kwa kuwa ni kilio cha wasanii cha siku zote.
CEO huyo kabla ya kuhamishiwa COSOTA alikuwa Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu kutoka Wakala wa Usajili wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).