KAMATI YA MIUNDOMBINU YAISHAURI SERIKALI KUKIKARABATI CHUO CHA DMI

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiomba serikali kukiongezea bajeti Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI)  ili kuweza kufanya ukarabati wa majengo na kukifanya kuwa cha kisasa kwakuwa majengo yaliyopo ni machakavu na  hayaendani na hadhi ya chuo hicho.

Akizungumza mara baada ya kamati hiyo kutembelea miradi mbalimbali iliyotekelezwa na chuo hicho,Mwenyekiti wa Kamati  hiyo Selemani Kakoso alisema baada ya kutembelea chuo hicho wamegundua wana vifaa na miundombinu za kisasa zakufundishia lakini shida ipo katika majengo ambayo ameeleza kuwa ni machache na eneo la chuo halina nafasi yakutosha hivyo amemuomba Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa kuhakikisha analisimamia hilo.

“Tunaomba waziri (Profesa Mbarawa) wasaidieni DMI waende katika maeneo ambayo watajitangaza sio hivi,chuo hiki kina vifaa vya kisasa vyakufundishia na kinatoa wataalam wazuri ambao wengi wao wanafanya kazi hadi nje ya nchi lakini majengo yao hayaendani na hadhi ya chuo chao.

“Chuo hiki wakipata Sh Bilioni 20 watakuwa hawakuulizi kitu wtakuwa wanatumia mapato ya ndani kujiendesha,tuna matumanini makubwa kwako  waziri muwasiaidie hawa ili waweze kulijenga Taifa,Kmati imejiridhishwa chuo kina miundombinu ya kisasa tatizo ni mazingira tukifanya maboresho kitakuwa kizuri,”alisema Kakoso.

Alisema wizara imekuwa ikijitahidi kusimamia vyuo vilivyo chini yake kwa kiasi kikubwa vyuo kwakuweka miundombinu yakufundishia kikiwemo Chuo Cha Usafirishaji (NIT) pamoja na Chuo cha Anga  lakink kumekuwa na tatizo la mazingira ya chuo kutokuvutia.

Alisema ni muhimu kurekebisha majengo ya chuo hicho kwakuwa ndiyo chuo cha kwanza kwanza Afrika Mashariki na pia kinapokea wanafunzi wengi kutoka nje ya nchi.

Naye Profesa Mbarawa alikiri kufahamu changamoto ya uchakavu wa majengo katika chuo hicho.

“Tunajua changamoto na tunafahamu umuhimu wa eneo hili tumefanya maamuizi TPA (Mamlaka ya Bandari) wanachukua eneo hili na wao ndo wanaenda kujenga chuo kinachojengwa Kimbiji,wao watachukua eneo hili kwa ajili yakujenga gati,”alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DMI Profesa Tumaini Gurumo alisema chuo kinaendela kufanya ujenzi wa matawi mapya yakiwemo ya Kigamboni na maeneo mengine.

Katika ziara hiyo wabunge walipata fursa yakuangalia vifaa mbalimbali vyakujifunzia vikiwemo full Mission Crane Simulator yenye thamani ya Sh  Bilionk 2.7,Mtambo wa meli ya mafunzo wakufundishia  Bilioni saba ambao umenunuliwa kwa ufadhili wa TPA.