Na Ibrahim Yassin
Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhani Kailima amewataka maafisa habari wa Serikali kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza zoezi lina lotarajiwa kuanza Julai 1,2024..
Kauli hiyo imetolewa jana wakati wa mkutano wa tume na maafisa habari wa mikoa na halmshauri uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
“Ndugu Maafisa Habari, uboreshaji huu unahusu kila mwananchi mwenye sifa, Tumieni njia mbalimbali kuelimisha jamii umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga awamu ya kwanza” Ndugu Ramadhani Kailima.
Awali akiwasilisha mada kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza, mkurugenzi wa Idara ya habari na elimu ya mpiga kura Giveness Aswile amesema zoezi hilo linatarajia kuanza Julai 01, 2024 na baada ya uboreshaji inatarajiwa kuwa daftari litakuwa na jumla ya wapiga kura 34,746,638.
“Katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kuzinga tia matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, daftari linatarajiwa kuwa na wapiga kura 34,746,638 kutoka 29,754,699 ya mwaka 2020 hili ni ongezeko la wapiga kura wapya 5,586,433 sawa na asilimia 18.7,” amesema Givennes
Ameongeza kuwa katika zoezi hilo wapiga kura 4,369,531 wanatara jiwa kuboresha taarifa zao na wapiga kura 594,494 wataondolewa katika daftari kwa kupoteza sifa za kuwa wapiga kura.
Akizungumzia kuhusu mfumo mpya saidizi unaofahamika kama Online Voters Registration System, (OVRS) amesema mfumo huu utawawezesha wapiga kura walioandikishwa kuanzisha mchakato wa uboreshaji kwa njia ya mtandao kupitia simu ya mkononi au kompyuta kubadilisha taarifa au kuhama jimbo au kata au kubadilisha na kuhama.
Hata hivyo baadhi wa wadau wmesema kutokana na umuhimu wa zoezi hilo ni bora waandishi wote wapatiwe magfunzo badala ya waliopo serikalini pekee.