WACHIMBAJI MADINI YA CHOKAA ZAIDI YA 300 WAOMBA KUKOPESHEKA KUONGEZA TIJA NA KUTUNZA  MAZINGIRA

Na Ibrahim Yassin,Songwe

KUNDI la vijana wanaojishughulisha na uchimbaji wa chokaa kijiji cha Nanyala wilayani Mbozi mkoani Songwe wameiomba serikali na wadau wengine kuwawezesha ili waweze kukopesheka kuongeza tija katika uzarishaji..

Kundi hilo la vijana zaidi ya 300 wametoa maombi hayo ili waweze kuchimba na kuchoma chokaa kisasa kwa kutumia makaa ya mawe ukilinganisha na hivi sasa wanavyochoma kwa kutumia kuni.

Wakizungumza jana na gazeti hili,wanasema njia wanazotumia zime tafsiriwa kuwa ni uharibifu wa mazingira kutokana na kutumia kuni nyingi zinazokatwa kwenye mapori hivyo wanaomba uwezeswaji ili watumie njia za kisasa.

Wanasema mfumo wanaotumia ni wa kizamani kwani wanachimba mashimo wanaingiza mawe kisha wanayachoma kwa magogo baada ya hapo wanaipua na kuanza kubonda bonda na nyundo kabla ya kusaga mashineni wakitumia nguvu kubwa maslai yakiwa kiduchu.

Fransis Siame mchimba shokaa,amesema wamekuwa wakitumia magogo ya kuni wanazozinunua mikoa ya jirani na wanapochoma kwenye mashimo ya kienyeji wanaipua na kuyasaga mawe hayo kwenye mashine ndipo wanapopata choka

Daud Mwanyerere mchimbaji wa chokaa Nanyara amesema licha ya kupata manufaa mengi hasa kipindi hiki cha utawala wa Rais Dkt,Samia wanaomba uwezeshaji wa mikopo ili waachane na kutumia kuni waweze kuagiza makaa ya mawe.

Kalantin Paul mchimbaji,amsema pamoja na mafanikio waliyonayo changamoto nyingine kwao ni soko la uhakika kwani kwa sasa wanauza kiloba cha kilo 25 wanauza Tsh,20650 bei ambayo haiwapi faida sana.

Japhet Kasewa mmiliki kiwanda cha kusaga chokaa amesema ili waweze kufanikiwa zaidi,wanaomba mfumo wa ruzuku iliyositishwa 2016,kwa sasa bado wanatumia miundombinu ya zamani wanabeba mawe kwenye machimbo kwa Tsh,95,000 kwa tripu moja.

Amesema wakibeba mawe eneo la machimbo kuleta kiwandani wana agiza magogo Iringa na Makambako kwa Tsh,550,000 tripu moja kugonga nyundo kuyaweka kwenye saizi moja mawe Tsh,15,000 tipa moja.

Afisa mtendaji wa kata hiyo,William Kota anasema uwepo wa machimbo eneo hili umeongeza fursa za kiuchumi katika kijiji kwani wageni wengi na mzunguko wa fedha upo.

Anasema kupitia ushuru wanaoukusanya kupitia machimbo hayo wameweza kujenga shule,zahanati na huduma zingine muhimu,hivyo endapo wachimbaji wataondolewa changamoto kijiji na mtu mmoja mmoja uchumi utakuwa juu.

”Wamiliki wa machimbo wamekuwa mstari wa mbele kuchangiashughuri za maendeleo ikiwemo kuogeza ajira kwa vijana wanaotoka kwenye eneo la uchimbaji na hata wa kutoka mikoa jirani,hivyo ni muhimu kufanyiwa mikakati ya kupatiwa mikopo waongeze tija mara dufu.

Nae Japhet Kasewa mmiliki wa kiwanda,anasema wapo zaidi ya miaka 10 katika eneo hilo,wanachakata chokaa na kuuza maeneo mbalimbali eneo wapo zaidi ya 300 ,serikali ikiweka nguvu uzarishaji utaongezeka na kwamba warudishe utaratibu wa mwaka 2016 wa kuwapatia ruzuku.

”Serikali imekuwa imeweka nguvu kwenye uchimbaji wa madini pekee huku kwenye chokaa wamesahau,ni bora wakageukia na machimbo ya chokaa na kuongeza uzarishaji,kutafuta masoko ya uhakika vipato vitakuwa kwa kasi.

Fransis Gewe afisa madini anayesiimamia eneo hilo,amesema chokaa inayochimbwa eneo hilo,inatumika kuchanganya na udongo (Jipsam) kutengenezea barabara,kukamatishia madini ya dhahabu na hata kwenye ujenzi.

Amesema wachimbaji wametoa maombi muhimu na yeye ameyachukua na kuyapeleka kwa afisa madini mkaazi mmkoa wa kimadini ili afikishe sehemu husika kufanyiwa kazi.

Diwani wa kata hiyo ya Nanyara George Msyani anasema uwepo wa machimbo fursa za kiuchumi zimeongezeka pia eneo hilo lina gesi asilia,maru maru,na chokaa,miaka ya nyuma wachimbaji walikuwa wakipewa ruzuku ambayo ilisitishwa miaka ya 2000 na kitu,

Msyani,ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi,anasema eneo la uchimbaji ni ekali 62 kuna kila sababu ya kuongeza eneo na jitihada zifanyike kurejesha luzuku na kuzungumza na taasisi za kifedha kuwapatia mikopo wachimbaji hawa.

Pia anasema suala la utunzaji wa mazingira ndiyo ajenda kuu ya serikali chini ya Rais Dkt,Samia,hivyo wachimbaji wawezeshwe ili waachane na kutumika kuni kuchomea mawe ya chokaa na badala yake watumie makaa ya  mawe hali itakayorahisisha kazi na kutunza mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *