Na Mwandishi Wetu
A L I Y E K U W A mfanyakazi wa Benki moja kubwa, maarufu inayotoa mikopo kwa wakulima nchini, (jina tunalo), amebainika kuwa amejipanga akishirikiana na tajiri mmoja kuanza kuichafua taasisi hiyo kupitia baadhi ya vyombo vya habari kinyume cha sheria.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo TAIFA TANZANIA inazo mtumishi huyo wa zamani amekuwa akitumiwa kwa ajili ya masilahi binafsi na mwenzake (Tajiri), ambaye naye aliwahi kufanya kazi katika taasisi hiyo na kisha kufukuzwa.
Kwa mujibu wa taarifa tulizopata kutoka kwenye chanzo chetu cha kuaminika ni kuwa mtumishi aliyefukuzwa kazi na kuzusha uongo juu ya Taasisi hiyo aliyokuwa akiifanyia kazi kwa lengo la kupata huruma ya wananchi yupo kwenye mipango ya kuendelea kutumia vyombo vya Habari hususani magazeti kwa kushirikiana na mwenzake aliyefukuzwa nae kazi (Tajiri) kuzusha uongo ili kuuaminisha umma kuwa alifukuzwa kazi kinyume cha sheria, ingali kwamba anajua taratibu zote za utumishi wa umma zilifuatwa baada ya yeye kutenda makosa ya kiutumishi na kupelekea kufukuzwa kazi.
Aidha chanzo chetu kiliendelea kueleza kuwa wahusika hao wawili wamekusudia kutumia fedha mpaka kuhakikisha lengo lao linatimia la kuendelea kuishafua Taasisi hiyo na viongozi wote wa juu wanaoisimamia.
Taifa Tanzania ilibisha hodi mpaka kwenye ofisi za Benki iyo maarufu inayotoa mikopo kwa wakulima na kukutana na mmoja wa wafanyakazi wa taasisi hiyo huku akikataa kuandikwa jina lake gazetini kwa kuwa sio msemaji wa taasisi hiyo.
“Unajua hawa watu wanaendelea kuhangaika yule dada dereva wakati anafukuzwa kazi alikuwa na watu wengine mmoja wapo… Yupo dada ambaye ana hela… Yeye anatokea kwenye familia yenye hela naye alifukuzwa pia.
“Yeye yule ndio ana-‘mfund’ kwa sababu anafikiria kwamba huyu (anamtaja jina), kesi yake inaweza kuangaliwa kwa jicho la huruma na jamii…
“Alishafukuzwa kazi siku nyingi sana, akakata rufaa mamlaka za juu akashindwa akaanza kukimbilia kwenye vyombo vya habari kuwachafua viongozi wote wa juu na Taasisi kwa ujumla.
“Lakini amekata rufaa tena kwenye ngazi ya mwisho kwa hiyo anasubiri uamuzi ndio maana tokea mwanzo uongozi ulisemea kuwa swala lake liko kwenye ngazi za rufaa.
“Ni kama vile mtu kahukumiwa mahakama ya Hakimu Mkazi akakata rufaa mahakama Kuu akashindwa akaanza kwenda kwenye vyombo vya habari kupata ‘public sympathy’.
Uchunguzi wa TAIFA TANZANIA ulibaini mhusika alifanya makosa mengi ya kukiuka Sheria za Utumishi wa Umma hata hivyo hayawezi kuwekwa wazi kwa sababu bado yapo kwenye ngazi za sheria.
Inaelezwa kuwa, sio kweli kwamba alifukuzwa kazi kutokana na yeye kuwa likizo ya uzazi bali imetokana na makosa aliyoyatenda wakati akiwa kazini.
Ikumbukwe kuwa Mei 13, 2022 akiwa dereva wa taasisi hiyo alimgonga mtu na kumuua katika kijiji cha Mganza barabara ya Nguruka-Kigoma na kufunguliwa kesi ya usalama barabarani namba 6/2022 katika Mahakama ya Wilaya ya Kigoma, alihukukiwa kwenda gerezani mwaka mmoja kwa kosa hilo la jinai au kulipa faini ya shilingi elfu hamsini. Ambapo alichagua kulipa faini na kuwa huru.
Hukumu hiyo ilitolewa tarehe 18/07/2022 na Hakimu K.M.Matembei ambaye ndiye Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Kigoma.