DAVID MATHAYO AWATAKA VIJANA KUTUMIA SOKA KWA MAENDELEO

Ashrack Miraji Same

Mbuge wa Jimbo la Same Magharib Dkt David Mathayo amewataka vijana wilayani humo kutumia fulsa ya michezo kuendeleza ushirikiano Kwa ajili ya shughuli za uzalishaji wa pamoja Ili kuleta Maendeleo katika wilaya hiyo

David Mathayo ameyasema hayo Leo Wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa Mashindano ya Mathayo Cup 2024 yaliyofanyika katika viwanja vya Ruvu Jimbo la same Magharib wilayani humo ambazo timu hizo zitatimua kivumbi Mwaka huu. kwenye Mashindano hayo na zaidi ya timu 75 zitashiriki Mashindano ya mpira wa Miguu.

Amesema msimu wa Mwaka Jana Wakati wa uzinduzi wa Mathayo Cup timu ambazo zilijitokeza 53 ukilinganisha na msimu wa pili, inaonesha vijana wanavyoamasika kwenye michezo timu hizo zitachuana kwenye Jimbo la same Magharib hivyo mshindi wa kwanza katika Mashindano hayo atakabidhiwa kitita Cha sh milion 7 na Mshindi wa pili atakabidhiwa milion 5, na Mshindi wa tatu atakabidhiwa milion 3 na Nusu na wanne atakabidhiwa milion 1

Sambamba na hayo yote Mhe Mathayo Aliendelea kusema Mashindano hayo yanatumika kuwahamasisha vijana kujitokeza Kwa wingi kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za Mitaa pia yanatumika kueleza kazi ambazo zimefanywa na serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa chini ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwakumbusha Miradi Mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa wilaya ya Same hasa katika jimbo la same Magharib, Ili watakapofanya uchaguzi wafanye uchaguzi Sahihi.

Katibu Mwenezi wa wilaya ya Same Mohamed Ifanda Ambaye ni Mgeni Rasmi kwenye Mashindano hayo amesema kuwa anampongeza Mbuge wa Jimbo Hilo David Mathayo Kwani Kwa Sasa Jimbo la Same Magharib linaelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha mapinduzi inayotekelezwa Katika nchi hii vijana wanapokuwa wanaitwa pamoja na wanafanya michezo kwani hawafikirii mambo mengine Bali ni wanafikilia michezo tu hii inawajengea mahusiano mazuri baina ya wao wenyewe na serikali

Niwaombe vijana mnaoshiriki Mashindano haya kuwa wanzalendo wa Taifa letu na wilaya Kwa ujumla pia Kuacha Mambo yasiyo mazuri kama uvutaji bangi uuzaji mirungi ukabaji tumieni michezo hili kubadili taswira ya Taifa letu michezo ni Ajira michezo inaleta fulsa Mbalimbali za Maendeleo hapa Nchin tumieni muda mwingi katika kujishulisha kwenye michezo hii ambayo imeanzishwa na Mhe Mbuge wa Jimbo la same Magharib David Mathayo Kwa lengo la kuwataka vijana wawe na fikra chanya Katika nchi Yao na kushirikiana Kwa pamoja katika kuleta Maendeleo amesema Ifanda

David Mathayo ameamua kuonesha vijana wa Jimbo la Same Magharib wana nguvu ya kucheza mpira kazi anayoifanya ni kubwa kupitia vijana hawa maana unaposema timu 75 wapo vijana Zaidi ya 2000 hili siyo jambo dogo ni jambo kubwa la kuigwa katika Mkoa wa Kilimanjaro

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Mathayo Cup ndugu Raphael Senkoro amesema michezo katika Jimbo Hilo inaweza kukuza vipaji vya vijana wa Same na kwamba michezo ni Afya, Ajira.

Pia Amempongeza Mh Mathayo Kwa kutambua kundi hili la vijana hasa wanaoshiriki michezo hii, huko kwenye maeneo Yetu niwaombe madiwani muwe mnafanya Kijiji Kwa Kijiji ikiwezekana hili itakapofika kipindi Cha Mathayo Cup kila Kata inakuja imejipanga Kwa ubigwa amesema Raphael Senkoro

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *