MENEJIMENTI YA MOI YAWAPA ZAWADI NA SHUKURANI WATUMISHI WAKE

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imetoa zawadi ya Sikukuu ya Krismas kwa watumishi wake  1052, ili kuwapa motisha ya kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa wagonjwa .

Zawadi hizo ambazo ni Kilo 15 za mchele, lita 2 za mafuta ya kupikia na vinywaji zenye thamani ya Tsh. 50,000 zimekabidhiwa leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kwa wawakilishi wa watumishi hao na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI,  Mhe. Balozi. Dkt. Mpoki Ulisubisya.

Akikabidhi zawadi hizo Dkt. Mpoki amesema kuwa menejimenti ya MOI imewapa motisha watumishi wake ya mkono wa Sikukuu ya Krismas kwa kutambua mchango wao mkubwa wa kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa.

“Menejimenti ya MOI tumetoa zawadi na shukurani hizi ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wenu mkubwa hususani wa kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa, pia tunaomba msheherekee sikukuu kwa amani na furaha”- amesema Dkt. Mpoki

Kwa upande wake, Mhudumu wa Afya wa MOI, Amina Makunga ameishukuru menejimenti ya MOI kwa kuwapatia zawadi hizo kwani ni inawapa morali na motisha ya kufanya kazi zaidi ya kutia huduma za matibabu kwa wagonjwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *