Na Ibrahim Yassin, Songwe
MKOA wa Songwe ni moja ya mikoa ya kimadini inayozalisha madini ya aina mbalimbali ikiwemo dhahabu ambayo yamekuwa na mchango mkubwa wa kutatua changamoto ya ajira kwa vijana na ukuaji wa Uchumi wa wilaya Songwe Mkoa na pato la taifa kwa ujuma.
Akiwa makamu wa Rais wakati wa utawala wa hayati Dkt,John Magufuli,Rais wa awamu ya sita Dkt,Samia Suluhu,alifika wilaya ya Songwe na kufanya mazungumzo na wachimbaji wadogo kupitia umoja wao ambapo alipokea kero mbalimbali.
Moja ya kero zilizotolewa ni ukosefu wa maeneo ya kuchimba madini kwani vijana kila eneo walilotaka kuchimba waliambiwa ni eneo la mtu hivyo ilipelekea maisha magumu kwa vijana na kupelekea kuingia kwenye uharifu na wizi.
Vikao mbalimbali vilikaliwa kujadili namna ya kuwasaidia vijana tangu Rais wa awamu ya tano Dkt,Magufuli na hatimaye kipindi cha Rais Dkt,Samia ndani ya miaka mitatu ya utawala wake vijana wamefanikiwa kukata kiu yao na kupatiwa vitalu 19 kati ya 35 walivyoomba na tayari wameanza kuchimba.
Upatikanaji wa vitalu hivyo umepelekea kupatikana kwa ajira za vijana ya 12,000 na kuondoa kabisa vitendo vya uharifu kwani kwa sasa vijana wote wamejiingiza kwenye uchimbaji na nafasi zingine kwenye tasnia hiyo.
Changamoto nyingine ilikuwa ni ukosefu wa soko la uhakika la kuuzia dhahabu kwani awali wachimbaji walikuwa wakisafirisha kienyeji kwenda kuuza kwenye masoko ya ndani ya nchi nan je ya nchi na kuhatarisha maisha yao huku serikali ikikosa takwimu sahihi za madini pamoja na tozo.
Halmashauri ya wilaya ya songwe ina migodi na uchimbaji mdogo wa Dhahabu Sehemu mbalimbali za wilaya ya Songwe kama Mgodi wa Shanta,Sunshine na Migodi mingine ya makaa ya mawe Iliopo Sehemu ya Magamba wilaya ya Songwe.
Soko la madini mkoani Songwe lipo wilayani Songwe ambapo dhahabu zote zinauzwa kwa bei elekezi na kudhibiti waliozoea biashara za ujanja ujanja watakasirika, watabeza na kuhujumu lakini Kamati ya Usalama Wilaya ya Songwe imejipanga kuwadhibiti.
Baada ya tarehe 8 Mei, 2019 lilitoka tangazo kwa atayeuza madini nje ya Soko la madini la mkoa atakuwa anatenda kosa la jinai na adhabu yake ni kutaifishwa mali, kufunga mwaka mmoja au vyote viwili kwa pamoja.
Mwaka 2020 kila siku kulikuwa na upatikanaji wa kilogramu tatu za dhahabu ambazo zitaleta mauzo ya shilingi milioni 270 na kwa mwezi itakuwa bilioni 6.7, fedha ya serikali itakuwa milioni 472 na halmashauri ni milioni 20.2 kwa mwezi.
Soko hili la madini litawasadia hasa wachimbachi wadogo kutambulika na kuzuia utoroshaji wa madini tuna Imani tatizo la kudhulumiana na kupunjana litakwisha hivyo nawasihi wote wanaohusika na sekta ya madini kulitumia.
Uongozi na wanachama wote wa chama cha wachimbaji wadogo wanapongezwa kwa kuonyesha nia na kukubali kulipokea soko hili madini, mmeonyesha uzalendo na sisi tutashirikiana nanyi, kwani tunatambua kuwa soko hili ni kiunganishi kati ya wauzaji na wachimbaji.
Mkoa wa Songwe una leseni 24 za utafiti wa madini, 101 uchimbaji mdogo, 5 za wachimbaji wa kati na kwa mwezi Machi Wilaya ya Songwe ilizalisha kilogramu za dhahabu 411.1.
Umuhimu wa soko la madini utakuwa ni uwepo wa soko la uhakika la madini ambalo litakuwa na malipo halali, soko litaondoa tatizo la kudhulumiwa na kupunjwa, Uwezekano wa kuibiwa hautakuwepo, bei itaratibiwa na serikali na hiyvo kumnufaisha muuzaji na mnunuzi na litawezesha uwepo wa takwimu za uhakika.
Tume ya Madini na wakala wa vipimo walipewa angalizo na uongozi wa mkoa kuhakikisha wanasimamia vifaa na taratibu zitakazotumika katika kupima madini hayo ili kuepuka malalamiko.
Katibu wa chama cha wachimbaji wadogo (SOREFA) Mkoani Songwe Elias Pangani anasema wachimbaji wadogo wako radhi na ni walipaji wazuri wa kodi ya Serikali, wanaipongeza serikali kwa kuanzisha soko la madini kwani wamekuwa wakihangaika kutafuta masoko ya uhakika.
Kuzalisha kitu bila ya uwepo wa masoko ya uhakika ni kazi ngumu, kwahiyo wazo la uanzishwa ji wa masoko ya madini ni jambo la kuungwa mkono, tunampongeza Rais Dkt,Samia Suluhu wakati akiwa makamu wa Rais ndiye muasisi wa wazo hili,huku mamlaka ya mapato nchini (TRA) wakiahidi ushirikiano.
Kwa mujibu wa tathmini ya uchumi ya mwezi ya Benki kuu ya Tanzania (BoT) ya mwezi April, mapato yatokanayo ya uuzaji wa dhahabu yameongezeka kwa $100 milioni (takribani Sh,223 bilioni) mwishoni mwa mwaka uliomalizika Machi, mwaka huu, ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Tathmini hiyo inaonyesha kuwa mapato yanayotokana na mauzo ya nje ya dhahabu yameonge zeka kwa kiwango cha dola bilioni 1.68 katika mwaka uliomalizika mwezi Machi mwaka huu, kutoka dola bilioni $1.53 kiwango kilichorekodiwa wakati wa mwaka uliomalizika Machi 2018.
BoT inasema kuwa uuzaji wa bidhaa nyingine katika nchi za nje huku waziri wa Madini,An thony Mavunde akiyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampuni za uchimbaji.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula anasema kuwa wamepokea maagizo na kwa Naibu waziri wa Madini Dkt,Steven Kirusi kuiagiza tume ya madini kutafuta masoko na tayari jitihada zimefanyika.
MAFANIKIO SEKTA YA MADINI WILAYA YA SONGWE
Wilaya ya Songwe ni wilaya moja wapo kati ya wilaya 5 nchini zenye postikodi namba 54100 (1) kitika sense ya mwaka 2022 wakazi waliohesabiwa ni 229,219,na makao makuu ya wilaya ni Mkwajuni ambapo kata ya saza ni maarufu kwa uchimbaji madini,kuna ngodi wa Shanta Gold Mine, Mbangala.
Ofisi ya madini ina jukumu la upokeaji na ushughulikaji wa maombi ya Leseni,vibali vya madini na baruti,ukaguzi wa shughuri mbalimbali za madini na huduma za ugani kwa wachimbaji wadogo,utoaji wa elimu kwa umma na huduma za ugani kwa wachimbaji.
Mkoa wa Songwe umejaliwa na aina mablimbali za madini ambayo ni madini ya Metali (Dhahabu) ,Fedha, Ofisi ya Madini Songwe ilianza ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali tarehe 01 Julai 2020 ikiwa inahudumia Wilaya zote za Mkoa wa Songwe ambazo ni Ileje, Momba, Mbozi na Songwe.
Ofisi ina majukumu ya upokeaji na ushughulikiaji wa maombi ya leseni, vibali vya mad ini na baruti; Ukaguzi wa shughuli mbalimbali za madini; utoaji wa elimu kwa umma na huduma za ugani kwa wachimbaji wadogo; ushughulikiaji wa kero na malalamiko kwenye maeneo ya madini.
Ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali katika sekta ya madini. ofisi pia inasimamia ofisi ya MRO – Shanta, na Kituo cha ukaguzi Madini- Tunduma,mkoa ya Songwe umejaliwa kuwa na aina mbalimbali za madini ambayo ni Madini ya Metali (dhahabu, fedha, shaba, risasi, chuma na madini ya kimkakati (Neodymium na Praseodymium)
Pia kuna Gesi ya Helium na Ukaa, Madini ya viwandani (Granite, Marble, chokaa na chumvi), Madini ya Vito (Fluorite, Mica na Sodalite), Madini ya Nishati (Makaa ya Mawe) na Madini Ujenzi (Mawe, Mchanga, Moramu na Kokoto).
Mkoa wa Songwe una leseni ya uchimbaji mkubwa (SMLs) 2, leseni za utafutaji mkubw a wa madini (PLs) 76, leseni za uchimbaji wa kati (MLs) 28, na uchimbaji mdogo wa madini (PMLs) 1050.
Mkoa wa Songwe una vinu vya uchenjuaji dhahabu (Vat Leaching Plants) 203 na Elution Plants 15, Aidha kuna leseni za wafanyabiashara wakubwa wa dhahabu (DLs) 25 na wafanyabiashara wadogo wa dhahabu (BLs) 140.
Utoaji wa leseni ndogo za uchimbaji madini (PMLs) umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na kutengwa kwa maeneo ya uchimbaji kwa ajili ya wachimbaji wado go.
UZALISHAJI WA UCHIMBAJI MDOGO NA UCHENJUAJI)KUPITIA SOKO LA MADINI SONGWE
Katika kipindi cha kuazia July 2020 ha Mei, 2024, ofisi ya Madini Songwe imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa madhuhuli ya serikali kupitia soko la madini Songwe kutoka kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu.
Wachimbaji wadogo wa dhahabu wameweza kuzalisha kiasi cha gram 4,155,716.45 zenye thamani ya shilingi bilioni 523.56 kutokana na uzalishaji huo, ofisi ya madini imeweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 36.63 (bilioni 31.41 mrabaha na bilioni 5.22 ada ya ukaguzi).
Mbali na hilo imeweza kuiwezesha halmashauri ya Wilaya ya Songwe kukusanya ushuru wa huduma kiasi cha shilingi bilioni 1.571,Uzalishaji wa dhahabu kupitia soko la madini wilayani Songwe.
Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo mkoani Songwe Emmanuel Kamaka anasema,mika mitatu ya utawala wa serikali ya awamu ya sita wamefanikiwa pakubwa katika kukuza pato lao na la Taifa kupitia sekta ya madini.
Anasema suala la ukosefu wa maeneo ya uchimbaji lilikuwa changamoto sugu,na kwamba waliweza kukaa vikao mbalimbali na Rais Dkt,Samia wakati akiwa makamu wa Rais na kujadili changamoto za skta ya madini.
Anasema alipoingia madarakani suala la kutatua changamoto za wachimbaji lilikuwa ni agenda yake kubwa na hivi karibuni wamepatiwa vitalu 19 hali iliyopelekea vijana wengi kupata ajira na kupunguza masuala ya uhalifu.
UZALISHAJI WA DHAHABU KWENYE SOKO LA MADINI SONGWE
Mwaka 2022/2023 Tsh,1,111,35 kitu ambacho ilikuwa ndoto kukusanya fedha hizo na kupitia mipango ya Rais Dkt,Samia kuweka mikakati hii miaka miatatu iliyopita hatimaye malengo yamekamilika.
MAFANIKIO NA MAKUSANYO YA MADINI MIAKA 3 YA RAIS DKT,SAMIA.
Luganziza Chone Malembo afisa madini mkaazi mkoani Songwe anasema ofisi yake imefanikiwa kusimamia utekelezaji wa sheria ya madini sura 123 kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ya serikali.