Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa wateja na wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha Maji Ruvu Juu siku ya Jumanne Julai 16 ,2024.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha DAWASA imeeleza kuwa huduma hiyo itakosekana kwa muda wa saa 15 yaani kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa tatu usiku.
Taarifa imeeleza kuwa sababu ya kukosekana kwa huduma hiyo ni kuruhusu matengenezo kwenye bomba kuu la kusafirisha maji ghafi kutoka Mtoni kwenda Mtamboni katika eneo la Mlandizi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo maeneo yanayoathirika ni Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn.
Maeneo menginie ni Mshikamano, Mbezi, Kimara,Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Msigani, Maramba Mawili, Tabata, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Ukonga, Pugu, Gongo la Mboto, Uwanja wa Ndege, Majumba sita , Kiwalani, Segerea, Kinyerezi na Kisarawe.
DAWASA imeomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.