Na Ashrack Miraji Lushoto Tanga
Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Mkoani Tanga,Jafar kubecha amewaomba radhi wananchi na wageni wote waliotarajia kuja kwenye tamasha la kitalii la “Usambara Tourism Festival” lenye lengo la kukuza uchumi hasa kwenye sekta ya utalii wilayani hapo.
Kubecha amesema tamasha hilo ambalo lilipagwa kufanyika Julai 25-27 mwaka huu kuwa limesogezwa mbele kutoka na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao,hivyo tamasha hilo litafanyika Septemba 6 – 7 mwaka.
“nitumie fulsa hii kuwapa pole wananchi na wageni wetu ambao tuliwatarajia kushiriki kwenye tamasha letu kuja kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii na majengo wakubwa ambayo yalijegwa na mjerumani hususani jengo la Mkuu wa Wilaya ya Lushoto” alisema Kubecha.