


WAPAMBE WAANZA RAFU ZA UCHAGUZI MOROGORO MJINI
Na Mwandishi Wetu,MorogoroWAKATI kipyenga cha uchukuaji fomu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo Urais, Ubunge na Udiwani kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuwapata wagombea wa kupeperusha bendera ya chama hicho kikiwa bado hata hakijapulizwa tayari michezo michafu ya inayohusishwa na rushwa imedaiwa kuanza katika jimbo la Uchaguzi la Morogoro Mjini. Hatua hiyo…

KATIBU MKUU UCHUKUZI AWATAKA WADAU KUTUMIA BANDARI KAVU YA KWALA
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam KATIBU Mkuu wa Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara amewataka wadau kuendelea kutumia bandari kavu ya Kwala kwani bandari hiyo inasaidia kupunguza msongamano wa foleni ya malori pamoja na mizigo katika bandari ya Dar es Salaam. Kahyarara amesema hayo kwenye kikao cha wadau wa bandari kilichofanyika jijini Dar es salaam na…

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI RUFANI THE CITIZEN DHIDI YA MCHECHU
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam MAHAKAMA ya Rufani ya Tanzania jana imetoa uamuzi wake katika Rufaa Namba 658 ya mwaka 2023, iliyowasilishwa na Mwananchi Communications Ltd pamoja na Mhariri wa The Citizen Newspaper dhidi ya Nehemia Kyando Mchechu, na kutupilia mbali maombi hayo kwa kukubaliana na maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyotolewa Machi 3, 2023. Katika…

UTENDAJI KAZI WA WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE WAIMARIKA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 95
Na Mwandishi Wetu,Dodoma Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewapongeza Watendaji wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kuendelea kuimarisha utendaji kazi na hivyo kuifanya Sekta ya Nishati kuwa na matokeo chanya katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo kufuatia tathmini ya utendaji kazi iliyofanywa na…

RAIS SAMIA AONGEZA AJIRA MPYA 300 TRA
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ameridhia kuongeza ajira mpya 300 za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kufanya jumla ya ajira zote kufikia 1,896 kutoka 1,596 zilizotangazwa awali. Nyongeza hiyo imetokana na ombi la TRA la kuongeza nafasi za ajira 300 ambazo zilikasimiwa kwenye…

WAZIRI DKT. GWAJIMA AANISHA VIPAUMBELE VITANO WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII 2025/26
Na Mwandishi Wetu, Dodoma Waziri wa Maendeleo ya Jamii. Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameainisha vipaumbele vya Wizara vikubwa vitano katika utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Dkt. Gwajima ameainisha hayo wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka husika wa Fedha jana Mei 27, 2025 Bungeni jijini Dodoma….

KAPINGA:MITAA 58 HALMASHAURI YA MJI WA TARIME IMEFIKIWA NA UMEME
Na Mwandishi Wetu,Dodoma Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali imefikisha umeme kwenye mitaa 58 ya Mji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kati ya mitaa 81 ya Halmashauri hiyo. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 26, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Tarime Mjini, Mhe. Michael Kembaki aliyeuliza Serikali…

TCB YAPATA FAIDA YA SH BILIONI 44
Na Aziza Masoud,Dar es Salaam BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imetengeneza faida ya Sh Bilioni 44 kabla ya kodi katika mwaka wa fedha uliopita huku ikisisitiza kuwa kiasi hicho ni kikubwa zaidi kuwahi kutokea. Akizungumza na Waandishi wa habari leo Machi 26, 2025 wakati wa mkutano wa 33 wa wanahisa wa benki hiyo Mkurugenzi Mtendaji…

WANANCHI LINDI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MADINI
Na Mwandishi Wetu,Lindi WANANCHI wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kuacha uvivu na badala yake wachangamkie fursa zilizopo kwenye sekta ya madini hususani katika mgodi wa kati wa Elianje uliopo kitongoji cha Namungo, Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Chingumbwa, kilichopo Kata ya Namungo, Abdallah Rashid akielezea fursa zilizopo…