VETA Karagwe inavyowakomboa vijana kupitia elimu ya ufundi

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu imeamua kuwekeza katika vyuo vya ufundi na ikapanua huduma zake katika Chuo cha VETA wilayani Karagwe ambapo awali kulikuwa na vyuo vya mkoa na vyuo ambavyo vilikuwa kwenye kanda.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika chuoni hapo Mkuu wa Chuo cha VETA Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Pascal Thomas,amesema kuwa,chuo hicho ni miongoni mwa vyuo wilayani humo na kinachotoa huduma bora.

Amesema kuwa wao Karagwe wapo kanda ya ziwa ambayo inaunganisha mikoa ya Mwanza,Mara,Kagera pamoja na Geita na katika Mkoa wa Kagera ambao una Wilaya ya Karagwe, Misenyi,Kyerwa ,Ngara ,Muleba,Biharamuro pamoja na Bukoba hivyo katika vyuo ambavyo vimepandishwa hadhi ni pamoja na chuo cha Karagwe ambapo chuo kihistoria kiliaza mwaka 1986 na kilikuwa kinamilikiwa na mtu binafsi ambaye alikuwa marehemu Edmin MkendaKenda.

Thomas amefafanua kuwa baada ya aliyekuwa mmiliki wa chuo hicho kuona gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa ndipo aliamua kukabidhi kwa Halmashauri ya wilaya hiyo tangu mwaka 1992 na kuanzia mwaka huo chini ya Halmashauri ya wilaya kiliendelea kutoa huduma ya mafunzo ya ufundi nchini hivyo mpaka sasa hivi kinaendeshwa na Serikali kwa asilimia mia moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *