Na Mwandishi Wetu,Arusha
Benki ya Stanbic Tanzania imetoa msaada wa viti 50 kwa Shule ya St. Jude ya jijini Arusha kuwezesha zaidi ya wanafunzi 1,800 wanaotoka kwenye familia zenye uhitaji kupata elimu.
Msaada huu ambao ni sehemu ya sera ya benki hiyo ya uwajibikaji, katika kurudisha kwa jamii sehemu ya faida yake (CSR), utaimarisha uwezo wa taasisi hiyo katika kutoa elimu bora, kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuwafikia watoto wengi zaidi wenye uhitaji.

Meneja wa Benki ya Stanbic, Tawi la Arusha, Hemed Sabuni aliwakilisha benki hiyo katika hafla ya makabidhiano jijini humo jana.
Amesema benki hiyo itaendelea kutoa misaada sehemu mbalimbali nchini kurudisha sehemu ya faida iliyoipata kwa jamii
“Jitihada hizi ni sehemu yakurudisha faida kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wenye uhitaji katika maeneo tofauti nchini. Benki ya Stanbic imekabidhi viti hivyo ili kuunga mkono juhudi za Shule ya St Jude ya kutoa elimu kwa watoto wenye ufaulu mzuri na vipaji lakini wazazi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za elimu,”alisema Sabuni.

Naye Mkuu wa shule ya St Jude, Ndaki Saguda aliishukuru benki hiyo na kuahidi kuvitunza viti hivyo ili viwasaidie wanafunzi hao.