MIZIGO YAONGEZEKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyrara amesema kuwa kwasasa katika Bandari ya Dar es Salaam kunaongezeko kubwa la Meli na Mizigo hivyo Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Kwa kushirikiana na Shirika la Reli (TRC) kuhakikisha wanaboresha Bandari Kavu ya Kwala.

Kahyarara ameyasema hayo jana Machi 25 mwaka 2025 kwenye kikao kilichowakutanisha wadau wa Bandari ya Dar es Salaam kilichofanyika katika Makao makuu ya Bandari jijini Dar es Salaam.

“ Kwa sasa mizingo na Meli imeongezeka sana hivyo ni muhimu mizigo hiyo iamishiwe kwenye Bandari kavu ya Kwala, Mizigo ikienda katika bandari kavu Kwala tutaondoa changamoto ya Malori kwa Bandari ya Dar es Salaam” alisema Prof. Godius Kahyarara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Abedi Gallus amesema kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari inaendelea na mpango kuendelea kuondoa changamoto msongamano wa malori pia kuchukua eneo la APZA kwa ajili ya kufadhia makasha pia kuhakikisha mizigo mingine kuhamishiwa katika Bandari ya Kwala.

“ Kwa sasa TPA imejipanga kuhakikisha inapunguza msongamano wa Malori pamoja na mizigo katika bandari ya Dar es Salaam, kwa kuhamishia mizigo kwenye Bandari ya Kwala pia eneo lililokuwa la APZA kuliboresha na kufikia kwezi wa Disemba tulitumie kwa kutunza Makasha, alisema Gallus.

Naye Mkurugenzi Mkurugenzi wa Sekta Binafsi Bw.Raphael Maganga amesema kuwa ni muhimu kuboresha bandari ya Kwala ili kuondoa Msongamano wa Malori na Sherehena ya Bandari ya Dar es Salaam hivyo itaongeza watumiaji katika Bandari ya Dar es Salaam

Kikao cha Mabaoresho ya Bandari inawakutanisha watau mbalimbali wanaoutumia bandari hiyo kama vile Sekta binafsi, TPA, wizara ya Uchukuzi, TBS, TPFS, TRA,Central Corridor na Mawakala wa Forodha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *