PROFESA MBARAWA:ATCL YAANZA RASMI KWENDA KINSHASA

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

SERIKALI kupitia Wizara ya Uchukuzi imezindua rasmi safari za ndege ya Air Tanzania kati ya Dar es Salaam, Tanzania na Kinshasa, DRC ambapo hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wawekezaji, na Mabalozi

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Prof Makame Mbarawa ametoa pongezi kwa Viongozi Wakuu wa Nchi mbili kwa maono haya ambapo yameandika historia mpya katika mashirikiano.

Alisema uzinduzi huo ni hatua kubwa katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na DRC na ni ishara ya uanzishwaji wa dira mpya ya ushirikiano wa kikanda

“Uzinduzi huu ni zaidi ya tukio la usafiri, ni ishara ya ushirikiano mpya utakaofungua fursa nyingi za biashara, kukuza utalii na ajira kwa wananchi wa nchi zote mbili ” amesisitiza Mbarawa.

Aidha Mbarawa ameipongeza Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) kwa kufanikisha safari hii mpya, na kuhimiza umuhimu wa kutoa huduma bora kwa abiria na kuhakikisha usalama wa hali ya juu.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi kutoka DRC Mhe Paul akimuwakilisha Djunga Waziri wa Uchukuzi wa Nchi hiyo na Naibu Waziri Mkuu Mhe Jean Pierre Bemba ameongeza kuwa hatua hii ni mwanzo mpya wa ushirikiano thabiti baina ya mataifa hayo mawili jirani na ni kiashiria cha safari ya matumaini, maendeleo na mshikamano wa bara Afrika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mha Peter Ulanga amesema safari hizi zitakuwa zikifanyika katika siku nne za wiki ambazo ni jumapili, jumatatu, jumatano na ijumaa na itatumia masaa matatu na dk 20 ambapo itapunguza muda wa safari kati ya kinshasha, Kongo na Dar es salaam, Tanzania na kufungua fursa za kiuchumi kikanda

Vilevile maeneo mengine ambayo ATCL inaenda, Kinshasa utakuwa ni mji wa pili ambao inafanya safari zake mwingine ni Lubumbashi na kampuni itaendelea kutanua wigo ili kufikia vituo vingi zaidi vya Kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *