SERIKALI YAPANUA USHIRIKI WA WATANZANIA SEKTA YA MADINI
Na Asha Mwakyonde, DODOMA WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imefanya marekebisho ya Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania za mwaka 2018 ambapo Tume hiyo mara kwa mara itatangaza kupitia Kanuni ya 13A orodha ya bidhaa na huduma ambazo zinatakiwa kutolewa na kampuni za Kitanzania ambazo zinamilikiwa kwa asilimia 100…

