Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) dawa mpya za kulevya zinatengenezwa kwa kasi kubwa duniani ambapo mpaka sasa zimeshabainika dawa zaidi 1400.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika semina ya wadau wa DCEA Kamishna Msaidizi wa Sayansi Jinai wa Ziliwa Machibya alisema kumekuwa na ongezeko la dawa mpya duniani ambazo hazipo kisheria ambapo wahusika wanaotengeneza dawa hizo lengo lao ni kukwepa sheria ili na waendelee kuzitumia na kufanya biashara hiyo.

“Dawa hizi zinatengenezwa na watalaam katika nchi mbalimbali baada yakuona dawa zilizopo kisheria zinakamatwa katika maeneo mbalimbali,mpaka sasa zimeshagunduliwa zaidi ya 1400 dawa hizi ni hatari sana kwa vijana,”amesema Kamishina Msaidizi Machibya.
Amesema utengenezwaji wa dawa hizo si salama kwakuwa unatumia kemikali bashirifu hivyo endapo kijana atatumia dawa hizo uraibu wake unamfanya kuwa na mabadiliko mbalimbali kwenye mwili ikiwemo macho mekundu.
Amesema ni wakati sasa jamii kuendelea kupambana na dawa za kulevya ikiwemo dawa hizo mpya zinapoingia nchini ili kuokoa kundi la vijana ambalo limekuwa likiathirika kwa kiasi kikubwa.


